Thursday 14 March 2013

CHIRIKU ORIGINALI APOTEZA MWANAE KWA MARA NYINGINE....


MWIMBAJI mwandamizi wa kundi la Jahazi Modern Taarab, Hadija Yussuf kwa mara nyingine tena amejifungua lakini mtoto amekuwa si rizki.
Hadija Yussuf alijifungua mtoto wa kiume katika hospitali ya Muhimbili leo asubuhi lakini mtoto huyo alifariki muda mfupi baadae.
Mume wa Hadija Yussuf, Khatib ameiambia mtandao wa Saluti5 kuwa mazishi ya kichanga hicho yamefanyika mchana huu kwenye makaburi ya Tambaza jijini Dar es Salaam.
Hii inakuwa ni mara ya nne kwa Hadija Yussuf (pichani) kufiwa na mtoto wakati wa kujifungua, mara ya mwisho ilikuwa ni katikati ya mwaka jana ambapo aljifungua kwa njia ya operesheni lakini mtoto akafariki.
Awali mwimbaji huyo alishauriwa na madaktari kupumzika kubeba mimba angalau kwa miaka miwili au mitatu jambo ambalo Hadija Yussuf ameshindwa kulitekeleza.
Moja ya sababu kadhaa zinazotajwa kuwa tatizo kwa Hadija Yussuf ni unene pamoja na uzito mkubwa.
Aidha wataalam wa mambo ya uzazi wanasema lilikuwa ni jambo la hatari kwa mwimbaji huyo kubeba mimba miezi michache tu baada ya kufanyiwa operesheni.
Kwa sasa Hadija Yussuf ana mtoto mmoja tu wa kike mwenye umri wa 16 aliyezaa na Seif Magwaru, mweka hazina wa Jahazi Modern Taarab.
Kwa hisani ya Saluti5....The screen masters.

Monday 11 March 2013

MZEE YUSUF AFUNGUKIA UTAJIRI WAKE, SKENDO YA USHIRIKINA.....

Big Daddy A.K.A Mfalme Mzee Yussuf

Hatimaye Mfalme Mzee Yusuf afunguka juu ya utajiri wake na skendo ya ushirikina ambayo imekuwa ikielekezwa kwake kupitia mtandao mmoja wa burudani.

Mzee Yusuf ni Mkurugenzi wa Jahazi Modern Taarab ambayo aliianzisha rasmi mwaka 2006, maskani yake yakiwa jijini Dar.

Mzee Yusuf na kundi lake wamejipatia mafanikio makubwa katika medani ya muziki wa taarab na kurudisha hadhi ya muziki huo ulioanza kupoteza mvuto miaka ya 2000.


Swali: Kwanza Mzee Yusuf unazungumziaje muziki wa taarab?
 

Mzee Yusuf: Zamani muziki wa taarab ulikuwa na mashabiki hasa kipindi kile cha ushindani wa marehemu Nasma Khamis na Hadija Kopa. Walijitahidi sana kuupandisha kwenye chati lakini baadaye ukapotea ila kwa sasa tumeweza kuwarudisha mashabiki wetu na muziki unapendwa Tanzania nzima, siyo Pwani pekee kama ilivyokuwa zamani.

Swali: Inafahamika kuwa wewe ni miongoni mwa wasanii wenye mafanikio na utajiri mkubwa Bongo. Nini siri ya mafanikio yako?

Mzee Yusuf: Ni kweli mafanikio ya kundi langu yamekuwa yakiongezeka kwa kujipatia mashabiki kila kukicha. Umaarufu wake nao umekuwa ukiongezeka kila siku kwani sisi hatubagui mashabiki.


Huwa tunawafuata hadi Uswahilini kwa sababu ndiko kwenye mashabiki wengi ambao hawawezi kupanda teksi kuifuata bendi mjini. Wakati mwingine huwa tunapiga shoo za ‘ndondo’ (mtaani), harusi na sherehe mbalimbali za watu binafsi tena kwa gharama nafuu. Hiyo ndiyo siri ya mafanikio yetu.
 

Swali: Vipi kuhusu skendo ya ushirikina ambayo imekuwa ikielekezwa kwako?

Mzee Yusuf: Ushirikina upo sana hasa katika muziki wetu huu na tena ukiuendekeza basi utakutawala. Wengi wanaoamini kuwa hakuna mafanikio hadi kwenda kwa waganga huwa hawafanikiwi kabisa zaidi ya kuliwa fedha na waganga wa mjini na wengine wakishafanikiwa husahau maagano. Kwangu mimi hayo ni maneno tu, uchawi wetu ni kujituma katika kazi.
 

Swali: Je, ulishawahi kwenda kwa sangoma?

Mzee Yusuf: Siwezi kusema uongo kuwa sijawahi kwenda kwa mganga, nilishawahi kwenda tena nakumbuka wakati nazindua bendi yangu ya Jahazi mwaka 2006 pale Travertine Hotel, Magomeni, Dar.
Nilikwenda kwa mganga mmoja hivi maarufu sana nikamwambia nahitaji watu wajae kwenye uzinduzi, akaniambia watakuja watu elfu moja, nikamwambia nataka watu mia saba tu kwa sababu bendi yangu bado changa.

Mganga aliniambia nimpe laki tatu, ukweli sikuwa nayo ilibidi niweke bondi tivii yangu. Baada ya wiki moja, yule mganga akaniuliza kama nimetangaza huo uzinduzi kwenye vyombo vya habari na kuweka matangazo ya barabarani, nikamjibu ndiyo ila nilijiuliza sana kwa nini aniulize wakati alinihakikishia kuwa shoo itakuwa nzuri?

Siku ya tukio ilikuwa balaa, kwanza mvua kubwa ilinyesha watu wakanyanyua viti kujikinga, watu tuliowategemea hawakuja, ukweli nilipata hasara ambayo sikuitegemea, nikagundua kuwa kwenye muziki hakuna uchawi.....

Na habari ndiyo hiyo.

Kwa hisani ya GP.......




Sunday 10 March 2013

FUNGA KAZI/5 STARS KUIBUA ALBAM MPYA HIVI KARIBUNI.....

Funga Kazi Modern Taarab
KUNDI jipya la mipasho kutoka Dar es Salaam Tanzania, Funga Kazi Modern Taarab, linatarajiwa kuibuka na album ya pili hivi karibuni.

Baadhi ya vibao vitakavyokuwemo katika album hiyo ni kile kinachokwenda kwa jina la 'Udugu Kazi' kitakachoimbwa na Sheshi Beshi Zainab Machupa chini ya wanamuziki mahiri, Omar Kisila, Ramadhan Kisolo na Mussa Bass.

Mkurugenzi Mkuu wa Funga Kazi, Karya Temba ‘Kapteni Temba anadokeza kuwa kibao hicho ni maandalizi ya albamu yao mpya inayotarajiwa kutinga sokoni baadaye mwaka huu.

“Kibao hicho naamini kitafanikiwa vilivyo kuwashika mashabiki pamoja na wapenzi wetu wengi, kutokana na namna kilivyobeba ujumbe mzito na mpangilio mzuri wa vyombo,” anasema Temba. 

Haya yanajiri baada ya bendi hilo kukamilisha album yao ya kwanza kwa kina la 'Funga Kazi.'

5 Stars Modern Taarab
Na huku hayo yakijiri....Kundi lililosukwa upya hivi karibuni la 5 stars pia linapanga kupakua vibao vipya hivi karibuni.

Vibao vitakavyokuwa katika album hiyo mpya ni pamoja na ‘Ukurasa Mpya’ (Ally J), ‘Mwomba Mungu Hatoki Mtupu’ (Mwanahawa Ally) na ‘Jipange Upya’ (Mariam Hamdan).

Pia kundi hilo linapanga kujitambulisha rasmi mwezi ujao sambamba na kuzindua album hiyo mpya.  

Additional Information....Saluti5 (The screen masters) 


Tuesday 5 March 2013

LEILA RASHID AJIFUNGUA MTOTO WA KIKE......

Lujaina.
MKE wa Mzee Yussuf, Malkia Leila Rashid jana jioni alijifungua mtoto wa kike.

Leila alijifungua katika hospitali ya Dr Hameer iliyopo kariakoo na hali yake pamoja na mtoto ni nzuri.

Mzee Yussuf aliiambia Saluti5 (Mtandao wa burudani) kuwa Leila na mwanae wataendelea kuwepo hospitalini hapo kwa siku mbili tatu.

Kwa mujibu wa Mzee Yussuf, jina la mtoto (pichani) ni Lujaina.

 “Dua la mke wangu limepokelewa, alikuwa anaomba sana apate mtoto wa kike” alisema Mzee Yussuf.

Kwa hisani ya Saluti5.....The Screen Masters.


Sunday 3 March 2013

UPCOMING ARABIC & INDIAN RELEASES 2013.....


A LADY WITH CONFIDENCE - KHADIJA KOPA......

Khadija Kopa akifanya makamuzi

Bendi la Tanzania One Theatre TOT kutoka Dares salaam Tanzania lipo mazoezini kwa sasa kuandaa album zao mpya.

Katika mahojiano ya kipekee na Pwani FM, mmoja wa waimbaji katika kundi hilo, Malkia wa Mipasho Bi. Khadija Kopa amefichua kuwa moja wapo ya vibao katika album hiyo itaitwa ‘A lady With Confidence.’

“Album ndio ziko jikoni hivi sasa tunazipika na tuko katika kutizama tizama mashairi, shairi gani litamfaa mwimbaji gani ila kwa sasa tumeanza kutengeneza nyimbo kadhaa pamoja na Hemedi Omari kwahivo siwezi kusema mengi,” Akasema Khadija Kopa.

Akikichambua kibao chake kipya kilichorushwa hewani kwa mara ya kwanza jijini Mombasa Kenya kupitia Pwani FM Bi. Khadija alisema;

“Nyimbo hii inazungumzia jinsi ya kumwelekeza mwanamke ili amvutie mumewe, Hii nyimbo kama ya mafunzo upande mwingine na mwanamke anatakiwa awe na maneno mazuri kwa mumewe, Mwanamke kila wakati anatakiwa awe smart mbele ya mumewe sababu kujipodoa sio ujinga wala sio ubishoo ni fakhari ya mwanamke na tunastahili tuwasikilize waume zetu tuzungumze na wao vizuri tuwapeti peti unajua mwanamume ni kama mtoto mdogo sio anatakiwa kubembelezwa,” Alisema Commando wa uhakika Bi. Khadija Kopa.

MASHAUZI CLASSIC KUJITOSA KATIKA TAMASHA LA COAST NIGHT.........

Mashauzi Classic Modern Taarab
Bendi la Mashauzi Classic A.K.A Wakali wa kujiachia kutoka Dares Salaam Tanzania watahusika katika tamasha la COAST NIGHT linaloandaliwa kila mwaka katika ukumbi wa KICC huko jijini Nairobi tarehe 28 mwezi huu.

Taarifa zaidi zinafuata.....