Sunday 30 September 2012

MZEE YUSSUF NA KHADIJA KOPA KUKUTANA ANA KWA ANA USIKU WA LEO....

Macho yote usiku huu wa leo yatakuwa kwa mahasimu wawili katika tasnia ya taarab yaani Mfalme Mzee Yussuf na Malkia wa Mipasho Bi. Khadija Kopa watakapokuwa wanashiriki katika onyesho la aina yake katika ukumbi wa Travertine Hotel Magomeni huko jijini Dares Salaam Tanzania.

Onyesho hilo lililodhaminiwa na mtangazaji wa kituo cha radio Times (Tanzania) kwa jina la 'Dida' linatarajiwa kuanza saa tatu usiku wa leo mpaka cheee na litawashirikisha wasanii kibao wakali akiwemo Chidi Benz.

Haya yanajiri huku mambo yakionekana sio shwari kati ya Big Daddy A.K.A Mfalme Mzee Yussuf na Malkia wa Mipasho Bi. Khadija Kopa....

THABIT ABDUL KUFUNGA NDOA NA MWANAHAWA ALI CHIPOLOPOLO.....

Baada ya kuhusishwa kuwa na Jike la simba yaani Bi. Isha Ramadhan mara nyingi, Profesa wa Keybord Thabit Abdul Mkono wa Mwanaume Sherii nangai wa Mashauzi Classic anatarajia kumuoa muimbaji kutoka Kings Modern Taarab Mwanahawa Ally Chipolopolo A.K.A Rais wa machipukizi wa taarab Tanzania.

Akizungumza na Mwa4 kupitia kipindi cha 'Tam Tam za Mwambao', Thabit alisema tayari ameshatoa barua na sasa wapo katika maandalizi ya ndoa yao.
Pia Thabit anasema ana bonge la SURPRISE kwa kila mmoja ifikiapo mwezi Novemba mwaka huu.
Wakati huo huo wawili hao wameibuka na kibao kipya kwa jina la 'Hatuna Habari' kudhihirisha wazi wazi mapenzi yao yaani siku hizi mambo hadharani ama vipi?...Kutoka hapa tunawatakia kila la kheri katika maisha yao.
 

KUNANI KATI YA HASSAN ALI NA SAIDA MASHAUZI??

Ni jambo la kawaida kwa wasanii mbali mbali katika sanaa ya burudani kujitosa katika uhusiano wa kila aina na hasa wa kimapenzi.

Na si jambo geni kwa msanii kama huyu katika tasnia ya taarab kuwa katika uhusiano kama huo na mwenzake.

Namaanisha Young Hassan Ali na Dadake Isha Ramadhan maarufu kama Saida Mashauzi.

Hassan amethibitisha kuwa wawili hao walikuwa katika uhusiano wa kimapenzi lakini kwa sasa hamna tena kitu kati yao.

Japo aliongea kwa machungu, Hassan alidinda kusimulia chanzo cha kuvunjika kwa uhusiano wake na Saida  huku duru zikiashiria kuwa kuna mtu mwengine katika maisha ya bibi huyo.

Juhudi zetu za kumtafuta Bi. Saida Mashauzi zinaendelea.....na nitakujulisha zaidi.

VIDYA BALAN KUOLEWA NA SIDDHARTH ROY KAPUR MWEZI DISEMBA...


Kila mmoja katika ulimwengu wa Bollywood yuko katika pilkapilka ya kutafuta mchumba.

Baada ya Actor Saif Ali Khan na mwenzake Kareena Kapoor ambao wanaoana hivi karibuni, sasa inaonekana ni wakati wa actress Vidya Balan naye lakini na nani?

Si mwengine ila ni Siddharth Roy Kapur kama vile mnavyomuona hapo juu katika picha.

Wawili hao wamekuwa katika uhusiano wa kimapenzi kwa muda mrefu na sasa wanataka kuboresha zaidi uhusiano wao na duru zinasema kwamba huenda wakafunga ndoa mwezi Disemba mwaka huu.

Bi. Vidya Balan anasema, “I do believe in the institution of marriage. I will not ignore it for a long time. I will definitely get married.”

Japo hajazungumzia zaidi kuhusu tarehe ya harusi hiyo lakini mwezi Mei Bi. Vidya alithibitisha kuwa katika uhusiano na Siddharth.

 “I will admit that I am dating him but not beyond that,” Anasema Vidya Balan.

HATIMAYE PICHA ZA MJUKUU WA BACHCHAN ZANASWA KATIKA CAMERA....


Mwamuonaje mtoto jamaniiii? Ni waa si waaa?

Haiyaa huyu ndiye mjukuu wa Actor Amitabh Bachchan aliye pia kichuna cha Actor Abhishek Bachchan na Actress Aishwarya Rai.

Picha hizi zilinaswa kwa mara ya kwanza katika uwanja wa ndege wakati Bi. Aishwarya Rai alipokuwa akielekea huko Chicago kujiunga na mumewe Abhishek Bachchan aliye katika pilkapilka ya kuandaa filamu yake mpya  ‘Dhoom 3.’


Huku hayo yakijiri….Actor mashuhuri katika ulimwengu wa Hollywood maarufu kama Brad Pitt ana matumaini ya kufanya kazi na actress Aishwarya hata baada ya bibi huyo kukataa ombi lake mwaka wa 2004.
  
Na la kufurahisha ni kwamba actor huyo yuko tayari kufanya kazi na Bi. Aishwarya hata katika filamu ya kihindi kivyovyote vile ili mradi akate kiu yake.

Brad Pitt anasema, “The filmmaking, I hear, has evolved a lot in India and of late we have witnessed some good films making a presence at the Oscars and the world stage,” 

“That tells you a lot about the quality of the actors and the movies. You never know when I might decide to work in a Bollywood film and do one of those dance numbers with the whole crew in the backdrop.” 

 “Given a chance, I would like to work with Aishwarya Rai Bachchan because she's a versatile actor. She has worked brilliantly in films like ‘The Mistress of Spices', ‘The Last Legion', ‘The Pink Panther 2 ' and ‘Provoked' to name a few,”

“She is one of the most popular actresses of Bollywood, who has achieved huge acclaim in the west for her style, beauty and acting skills. I think we missed an opportunity to be cast together for the movie ‘ Troy ',” anasema Actor Brad Pitt.