Friday 26 October 2012

EID MUBARAK KWENU NYOTEEEEEEEE..........

EID MUBARAK
Mikono tupeane,

Rehema tutakiane,

Upendo tushikamane,

Toba tuhimizane,

Makosa tusameheane,

Yarabi tupe baraka zako,

Utukubalie swaumu zetu,

Amina yarabi Amina,.....


Nawatakia wasomaji wa Bloguu hii EID MUBARAK....KULLU '3AAM WAANTUM BIKHEYR....

Thursday 25 October 2012

KATWA KITU YAKO NA MALKIA WA MIPASHOOOO KHADIJA KOPA MWEZI UJAO HUKO MOMBASA........

Ni BAYANA kuwa Malkia wa Mipasho wa ukwee-eh Bi. Khadija Kopa atafanya ziara ya kipekee huko mjini Mombasa kuanzia mwezi ujao.

Lengo kuu ni kukupa wewe mpenzi wa taarab RAHA mpaka vichochoronii katika bonge la tamasha la 'Taarab weekend' litakalofanyika EXCLUSIVE huko TROPICANA CLUB.

Miongoni mwa vibao utakavyopata kuskia LIVE BILA CHENGA ni Mjini Chuo Kikuu, Full Stop, Top In Town miongoni mwa Mirindimo AJAB ya taarab....Chezea MAMA na majembe yake???UTALALA HOIII....Kazi kwako swahibaaaaaaaaa heheheyaaaaaaa...... 

Yatakayofuata NEXT:

MASHAUZI CLASSIC KUTUA MJINI MOMBASA MWEZI UJAO???????.....

NDOA YA MARIAM KHAMIS YAVUNJIKA,

MWASITI MBWANA ASIMAMISHWA KAZI KUTOKA JAHAZI,

THABIT ABDUL AIBUKA NA KANDA YA VIDEO YA KIBAO CHAKE LATEST ALICHOMSHIRIKISHA MWANAHAWA CHIPOLOPOLO 'HATUNA HABARI,'

BONGE LA TAMASHA KUFANYIKA MWEZI UJAO KUADHIMISHA ZAIDI YA MIAKA 10 YA KIPINDI CHA TAARAB 'MITIKISIKO YA PWANI' KINACHOMILIKIWA NA RADIO TIMES TANZANIA,
 
NITAKUPASHA MIKAKATI YA BENDI LA T MOTO YA KUZINDUA ALBAMU YAO (YA PILI) MPYA YA 'DOMO LA UDAKU' HUKO MJINI MOMBASA,

HATMA YA SULTWANI WA MIRINDIMO DR. MALIK IMEFIKIA WAPI BAADA YA KUFANYIWA UPASUAJI???....KAA MKAO WA KULA.
 



Thursday 18 October 2012

SALMAN KHAN AKO JUU KATIKA ULIMWENGU WA BOLLYWOOD…


Una habari kuwa actor huyu yuko juu kwa sasa katika ulimwengu wa Bollywood?

Si mwengine ila ni actor Salman Khan.

Inasemekana kuwa siku hizi actor huyu anafurahia maisha baada ya kuibuka kuwa miongoni mwa waigizaji wanaopata malipo ya hali ya juu katika ulimwengu wa bollywood.

Haya yanadhihirika baada ya filamu alizoshiriki hivi karibuni kama ‘Dabangg,’ ‘Ready,’ ‘Bodyguard,’ ‘Ek Tha Tiger,’ kufanya vyema katika charti ya filamu bora.
Huku hayo yakijiri, Pia Salman Khan ameonekana sana kukerwa na uhusiano wa karibu kati ya actor Shahrukh Khan na actress Katrina Kaif.

Uhusiano kati ya wawili hao (Shahrukh Khan & Katrina Kaif) unatokana na ujio wa filamu yao mpya "Jab Tak Hain Jaan' inayotarajiwa kutoka hivi karibuni.

Duru zinasema kuwa bado Salman Khan anamuenzi Bi. Katrina Kaif zaidi ya rafiki.

Haya yanajiri huku uhusiano kati ya wawili hao (Salman Khan & Shahrukh Khan) ukiendelea kufifia....Na habari ndio hiyoooo.