Tuesday 26 February 2013

LEILA RASHID KUJIFUNGUA HIVI KARIBUNI.....


MKE mkubwa wa Mzee Yusuf ambaye pia ni mwimbaji wa bendi la Jahazi Modern Taarab, Leila Rashid ‘’Malkia’’ anatarajia kujifungua muda wowote kuanzia sasa.

Kwa mujibu wa chanzo makini kilichoomba hifadhi ya jina lake, kwa kipindi kirefu Leila alikuwa haonekani kwenye bendi kutokana na ‘kuchoka’ na sasa ametimiza miezi tisa ambapo mumewe alimpumzisha kazini hadi atakapojifungua.

“Yah! Ni kweli mke wangu ni mjamzito na muda wowote kuanzia sasa anaweza kujifungua na baadaye atarejea kwenye bendi kama kawaida,” alisema Mzee Yusuf.

Monday 25 February 2013

KHADIJA KOPA AIBUKA NA KIBAO KIPYA MWAKA WA 2013......

Malkia wa mipasho Bi. Khadija Kopa commando wa uhakika kutoka Dar es Salaam Tanzania ameibuka na kibao kipya mwaka huu kwa jina la Fakhari ya Mwanamke na tayari kimeanza kuskika kupitia vituo mbali mbali vya radio ikiwemo Pwani FM.

Ni mojawapo ya vibao vipya vinavyoundwa kwa sasa chini ya bendi lisilo rasmi la G5 lililoko Dar es Salaam Tanzania. 

G Five ambalo limeundwa na wasanii wa bendi tofauti kama vile TOT Taarab, Mashauzi Classic, Jahazi Modern Taarab, Five Stars na New Zanzibar Stars, limetengeneza jumla ya nyimbo sita.

Kumekuwa na shaka kuwa huenda mkusanyiko huo ni ‘fitna’ mpya itakayopelea kuzaliwa kwa bendi mpya ya taarab, kama ambayo historia inavyotukumbusha namna bendi za Zanzibar Stars, Five Stars na Mashauzi Classic zilivyoanzishwa kutokana na mikusanyiko kama hii.

Mkusanyiko huu utaunda albam yenye jumla ya nyimbo sita.

Huku hayo yakijiri....
 
Bendi la T Moto tayari limekamilisha album yao ya tatu na kwa sasa linamalizia malizia vibao vitakavyokuwepo ndani.

Kulingana na mkurugenzi wa kundi hilo Amin Salmin, wanapanga kuzitambulisha nyimbo hizo katika vituo vya radio mbali mbali hivi karibuni.

Hii itakuwa albamu yao ya tatu baada ya kutambulisha ‘Domo la udaku’ na ‘Aliyeniumba Hajanikosea’.

SIKILIZA MAKALA YA ANA KWA ANA NA MWARI WA ZAMANI BI. RUKIA JUMA KUTOKA TOT/MASHAUZI CLASSIC MODERN TAARAB KATIKA KIPINDI CHA KWARAHA ZANGU NDANI YA PWANI FM....


Sunday 24 February 2013

FIVE STARS YATANGAZA KIKOSI CHAKE KIPYA.....

KUNDI la Five Stars Modern Taarab lililoko Dar es Salaam Tanzania wiki jana lilitangaza rasmi kikosi chake na kuwataka wapenzi wa muziki wa taarab wakae mkao wa kula.

Wasanii wapya wa kundi hilo walitajwa kwenye mkutano wa waandishi wa habari katika hotel ya Lamada ambapo Ali Jay alikuwa ni msemaji wa wasanii huku Jumanne Ulaya “J four” anakuwa mkuu wa juwkaa.

Wasanii wapya waliotajwa jana na bendi zao kwenye mabano ni Jumanne Ulaya (Msanii huru), Bi Mwanahawa Ali (East African Melody), Thabit Abdul (Mashauzi Classic / TOT Taarab) na Sabah Muchacho (Msanii huru).

Wengine ni Hammer Q (Offside Trick), Mosi Suleiman (Msanii huru), Mariam Amdani (East African Melody), Mariam BSS (Kings Modern Taarab), Mauwa Teggo na Yussuf Teggo (Coast Modern Taarab).

Ali Jay alisema kwasasa kilichobakia ni kwa wanamuziki hao wapya pamoja na wale wa zamani kuingia kambini kwaajili ya kutengeneza nyimbo mpya zitakazo tikisa ulimwengu wa wapenda taarab.

Naye Sharks ambaye ndie mmliki mpya wa kundi hilo, alisema kundi lake halina mpango wa kuanzisha malumbano na kundi lolote la taarab na litajitahidi kukaribisha ushirikiano na vikundi shindani kadri iwezekanavyo.

Kwa hisani ya Saluti5....The Screen Masters.

OFFSIDE TRICK WAIBUKA NA NGOMA MPYA......

Wakali wa ngoma za mduara kule Dar es salaam Tanzania wameibuka na vibao vipya kadha wa kadha ikiwemo 'Usinipe' ambapo wamemshirikisha Baby J katika album ya Nipe Nikupe.

Waambiwa...'Nakifungua kifua nanena yalotimia ee
Kamwe sitogombania pale nilopotokea
Nakifungua kifua nanena yalotimia ee
Kamwe sitogombania pale nilopotokea

Sili kisicholika ingawa kitu jamali
Na vyema kimepikika na kurashiwa asali
Madamu ni cha shirika kula sitokubali
Kamwe sitohadaika kwa kibakuli cha wali
Kula kitu cha shirika hairidhi yangu hali

Usinipe kinyama kinukacho moshi
mila zetu sie ni sumu ndani ya upishi .....'


Haya yanajiri siku chache baada ya msanii wa mduara Ali Tall maarufu kama AT kutoka Dar es Salaam Tanzania kutambulisha vibao vyake viwili mwaka huu kwa jina la 'Hana Haya' na 'Asali.'