Wednesday 30 January 2013

MASHAUZI CLASSIC WAKAMILISHA NYIMBO ZAO MBILI MPYA.......


Thabit Abdul akiongoza mazoezi ya nyimbo mpya jana

Isha Mashauzi mazoezini jana

Aisha Othman Vuvuzela


Hashim Said "Mzee wa Majanga"

Jumanne Ulaya "J Four" akipiga gitaa la solo
 


Saida Mashauzi akiimba mazoezini jana

Mpiga kinanda Kalikiti moto Mafia

KUNDI la miondoko ya taarabu, Mashauzi Classic limekamilisha nyimbo mbili kati ya zitakazounda albam yao mpya ijayo.

Kuanzia wiki iliyopita, kundi hilo lilianza rasmi mazoezi ya kutengeneza nyimbo zao mpya na katika hali inayoonyesha uwezo mkubwa wa wasanii wao kukamata nyimbo tayari vibao viwili “Mimi mwanaume” na “Ropokeni yanayowahusu” vimekamilika.

Saluti5 ilitembelea mazoezi ya kundi hilo jana na kukuta nyimbo hizo zikiwa katika hatua za mwisho kabla hawajaanza kugusa nyimbo nyingine.

Wimbo “Mimi ni Mwanaume” umeimbwa na Hashim Said “Mzee wa Majanga” huku ule wa “Ropokeni yanayowahusu” ukiimbwa na Aisha Othman “Vuvuzela”. Nyimbo zote mbili ni utunzi wake Thabit Abdul.

Kwa hisani ya Saluti5....The screen masters.

Tuesday 29 January 2013

SIKILIZA SEHEMU YA PILI YA MAHOJIANO YA ANA KWA ANA NA AT EXCLUSIVE NDANI YA PWANI FM.......KAZI KWAKO SASA


SIKILIZA SEHEMU YA KWANZA YA MAHOJIANO YA ANA KWA ANA NA AT EXCLUSIVE NDANI YA PWANI FM.......


MZEE YUSSUF AINGIA ‘LOCATION’ KUREKODI VIDEO YA WASI WASI WAKO...........

MKURUGENZI wa Jahazi Modern Taarab, Mzee Yussuf, leo anaingia chimbo kurekodi video ya wimbo wake mpya, “Wasi wasi wako”.
 
Kwa takriban wiki nzima kundi la Jahazi limekuwa mafichoni kurekodi video ya albam yao mpya ambapo kuanzia leo hii, ni zamu ya Mzee Yussuf kuingia kilingeni.

Mzee Yussuf ameimbia mtandao wa Saluti5 kuwa kwa mara nyingine anakuja na mabadiliko mapya ndani ya video yake kama alivyofanya katika wimbo wake uliopita wa Mpenzi Chocolate.

“Sijajua kazi hii itachukua siku ngapi, lakini mashabiki wetu waendelee kutegemea mambo mapya, tunabadilika kama kinyonga” alisema Mzee Yussuf.

Kwa hisani ya Saluti5....The screen masters....

Sunday 27 January 2013

MASHAUZI CLASSIC WAANZA MAZOEZI YA NYIMBO MPYA.....

KUNDI kabambe la miondoko ya taarab, Mashauzi, Classic limeanza rasmi mazoezi makali ya kutengeneza nyimbo mpya.

Mmoja wa wakurugenzi wa kundi hilo, Thabit Abdul, ameiambia mtandao wa Saluti5 kuwa nyimbo hizo ni maandalizi ya albam yao ijayo.

Thabit amesema wanakuja kivingine huku akiahidi kuwa safari hii nyimbo zao zitaleta mapinduzi makubwa kwenye muziki wa taarab, kuanzia upigaji pamoja na mpangilio wa mashairi.

Mazoezi hayo yanaendelea katika ngome yao Kinondoni Hananasif, jijini Dar se Salaam. 

Kwa hisani ya Saluti5....The screen masters.


Thursday 24 January 2013

KHADIJA KOPA AINGIA STUDIO NA G FIVE....

MALKIA wa mipasho, Khadija Kopa, jana aliingia studio za Sofia Production ili kurekodi wimbo wake mpya wa taarab chini ya kundi la G Five.

G Five ambalo limeundwa na wasanii wa bendi tofauti kama vile TOT Taarab, Mashauzi Classic, Jahazi Modern Taarab, Five Stras na New Zanzibar Stars, limetengeneza jumla ya nyimbo sita.

Mkurugenzi wa kundi hilo Hamis Slim alisisitiza kuwa kundi hilo si bendi ya kudumu bali mkusanyiko wa muda na kisha kila mtu ataendelea na bendi yake.

Hata hivyo kazi ya kurekodi wimbo huo mpya wa Khadija Kopa uliopewa jina la “Fahari ya Mwanamke” haikukamilika kutokana na hitilafu ya umeme.

Kutokana na tatizo hilo, Khadija Kopa sasa atalazimika kumalizia kiporo cha kazi iliyobakia leo mchana. 

Kwa hisani ya Saluti5....The screen masters
 

Friday 18 January 2013

LAMANIA SHAABAN: ‘MBUYU’ WA TAARAB ULIOACHA SIMANZI.....

HAKUWA mtu wa makuu na inawezekana wengi wakawa hawafamu uwezo wake wala sura yake …hakupenda kujikweza, lakini ni mtu mkubwa sana kwenye muziki wa taarab pengine kuliko yeyote unayemdhania wewe.
Marehemu Lamania Shaaban

Huyo ndie Lamania Shaaban aliyezikwa jana Tandika, Dar es Salaam huku akisindikizwa na mamia ya wasanii, wadau, ndugu, jamaa na marafiki waliopambwa na nyuso za huzuni.


Mwili wa Lamania aliyefariki juzi alfajiri ulipumzishwa katika nyumba yake ya milele majira ya saa saba za mchana.

Safari ya makaburini
Mwili wa Lamania Shaaban ukiingizwa kaburini
Mzee Yussuf ni kama haamini
 
Lamania aliyezaliwa mwaka 1969, mwenyeji wa Zanzibar, alikuwa ndiye mkurugenzi wa muziki wa East African Melody huku akiitungia zaidi ya nyimbo 40 ikiwa ni pamoja na kupanga mashairi na kutia sauti.


Lakini pia hata nyimbo zilizotungwa na watu wengine bado zilipita kwenye dawati lake na kuzifanyia uhariri. Alikuwa hana mpinzani katika gitaa la solo ndani ya Melody.


Alijiunga na East African Melody mwaka 1994 na kuanzia hapo akawa ni moja ya mihimili mikubwa ndani ya kundi hilo.
Mkurugenzi mkuu wa East African Melody, Hajj Mohamed akihojiwa na Hawa Hassan wa ITV
Watoto wa  Lamania Shaaban kutoka kushoto: Fatma, Mohamed, Nasria, Nasra na wa nyuma ni Shaaban

Wasanii kama Mzee Yussuf, Hajj Mohamed, Khadija Kopa, Bi Mwanahawa Ali, Hassan Soud, wote kwa nyakati tofauti waliiambia Saluti5 jana msibani kuwa Lamania ni pengo kubwa katika muziki wa taarab ambalo litachukua muda mrefu kuzibika. 

Huku hayo yakijiri....MWIMBAJI wa taraab wa Kings Modern Taarab, Hanifa Maulid, amsema licha ya kuvuna elimu ya uimbaji lakini pia marehemu Lamania Shaaban amemwachia kumbu kumbu kubwa.
 
Akiongea na Saluti5 jana, Hanifa alisema alibahatika kuishi maisha ya ndoa na Lamania ikiwa ni pamoja na kuzaa nae mtoto mmoja wa kike.

Enzi hizo marehemu Lamania na Hanifa Maulid
Hanifa Maulid akiwa na mtoto wake Nasra Lamania

Amesema japo baadae aliachana na Lamania, lakini mtoto huyo Nasra Lamania ndiye kumbukumbu pekee aliyoachiwa na mume wake huyo wa zamani.


Nasra anayesoma darasa la kwanza anaungana na watoto wengine wanne wa Lamania kutoka kwa mama mwingine kuunda jumla ya watoto watano waliachwa na marehemu. 
 
Kwa hisani ya saluti5...The screen masters.

MDOGO WAKE ALLY STAR ALIYETESEKA KITANDANI KWA MIAKA 8 AFARIKI DUNIA...

Ally Star....
MDOGO wake na mwimbaji wa TOT Taarab, Ally Hemed Star, amefariki jana jijini Dar es Salaam baada ya kuugua kwa muda mrefu.
 
Marehemu aliyejulikana kwa jina la Abdallah Hemed, anategemewa kuzikwa Ijumaa ya leo asubuhi nyumbani kwao Kilosa mkoani Morogoro.

Ally Star ameiambia Saluti5 kuwa waliondoka Dar es Salaam jana jioni kwa gari la TOT, kuelekea Kilosa kumhifadhi mdogo wake mpendwa.

Kufariki kwa Abdallah Hemed ambaye ndiye anayemfuatia Ally Star kwa kuzaliwa, ni matokeo ya kuugua kwake ugonjwa wa kupooza uliomlaza kitandani kwa miaka minane.

Siku kadhaa zilizopita, Saluti5 ilifanya mahojiano marefu na Ally Star ambapo alizumgumzia jinsi maisha ya kumuuguza mdogo wake yalivyo.

Akimzungumzia mdogo wake wiki chache zilizopita kupitia Saluti5, Ali Star alisema: Kwa kujibana sana gharama za dawa kwa kila wiki ni sh.57,000, mwaka wa nane sasa anamhudumia mdogo wake ambaye anaishi nae nyumbani kwake.

“Pesa zinazoingia ni kidogo, zinazotoka ni nyingi, naumia sana kwa kumuona mdogo wangu anateseka kitandani, lakini naumia zaidi pale ninapohisi kuwa wakati fulani mi si msaada wa kutosha kwake.

“Wakati mwingine unatembea barabarani unaongea peke yako kama chizi, natamani siku moja nipate japo neno moja kutoka kwa mdogo wangu lakini Mungu alishamfunga kauli siku nyingi, hana uwezo wa kufumbua mdomo na kuongea lolote, tunatazamana kama picha tu.

“Maisha ya Hospital yameshindikana, kwasasa matibabu yote yanafanyika nyumbani, hata chakula chenyewe ana kula kwa mrija, kila siku hali inazidi kukatisha tamaa” hiyo ndio ilikuwa kauli ya Ally Star.

Ally Star ameiambia Saluti5 kuwa anaushukuru uongozi wa TOT, wasanii wenzake na wadau wote walifanikisha safari ya kwenda Kilosa kumzika mdogo wake.

Kwa hisani ya Saluti5....The screen masters.


Wednesday 16 January 2013

AT AIBUKA NA GOMA MPYA YA MDUARA 'HANA HAYA'.......

Mwimbaji wa Mduara na Kizazi kipya Ali Ramadhan 'AT' ameibuka na kibao chake kipya cha mduara mwaka huu wa 2013 kwa jina la 'Hana Haya.'

Safari hii AT alimshirikisha Bi. Salha Abdallah kutoka kundi la taarab la Dar es Salaam Modern Taarab katika kibao hicho.

Baadhi ya vipande katika kibao hicho ni kama.... "Wapi tena mwenzangu? Nenda kwa waziri wa umbeya na mambo yasiomhusu mheshimiwa hana haya...Makubwaaaa!!!...Yaliomshinda viumbo kunyang'anyua ukubwa kwa kugombea ubwabwa." 

Hivi sasa anajiandaa kukamilisha mkanda wa video yake na utaiona SOON......

Haya yanajiri huku kundi la 'Offside Trick' likimshirikisha Baby J likitarajiwa kuachia kibao chao kipya kwa jina la 'Usinipe' hivi karibuni.

MISAMBANOOOO ANASEMAJEEEE????......SHAABAN LAMANIA KIONGOZI NA MTUNZI WA EAST AFRICAN MELODY AFARIKI DUNIA.....

MWIMBAJI wa taarab na muziki wa dansi, Abdul Misambano “Super Rocks” amempongeza mkurugenzi wa Jahazi Modern Taarab, Mzee Yussuf kwa kuthubutu na hatimaye kufanikiwa kuunda kundi la Jahazi.
 
Misambano anayelitumikia kundi la TOT, aliyasema hayo alipokuwa anahojiwa na Hawa Hassan katika kipindi cha Sham Sham za Pwani cha ITV, Jumatatu usiku.


Alisema anampongeza kwa vile wako waimbaji wengi waliopata nafasi kama ya Mzee Yussuf lakini walishindwa kuzitimia.

Mwimbaji huyo aliyepata kutamba na wimbo wa “Asu” aliouimba akiwa na Babloom Modern Taarab, anamtaja Ali Hemed “Star” kama moja ya mifano yake.
 
“Enzi za Ali Star, nilishuhudia mwimbaji huyo akituzwa kapu la pesa, alikubalika sana na angeweza kabisa kuanzisha kundi lake na akafanikiwa lakini kwa bahati mbaya hakuthubutu.


“Mzee Yussuf alithubutu na akafanikiwa na pia ameweza kuzalisha wasanii nyota kama Isha Mashauzi na wengine wengi, kwahiyo nampongeza sana” alisema Misambano.



Misambano pia alishutumu tabia ya waimbaji wa sasa wa kiume kwa kuigana sana sauti kiasi cha kufikia hatua ya kushindwa kuwatofautisha.


“Zamani akiimba Misambano, Hussein Kibao, Ali Star, Mohamed Mrisho au Ali Taajiruna hutapata shida, kila mtu na sauti yake na staili yake.


Kizazi cha mwisho kukiona kikifanya kivyo ni Mzee Yussuf na marehemu Omar Kopa, walikuwa hawafanani, lakini baada ya hapo imekuwa taabu, ukimsikiliza Omar Teggo na Mzee Yussuf ni mle mle hakuna tofauti.


Huyu mtoto mpya wa Jahazi (Mohamed Ali) akiimba ni kule kule kwa Mzee, Amigo anajaribu kubadilika lakini bado kuna sehemu anapita pale pale kwa Mzee Yussuf, watu wanaigana sana” alisema Misambano.
Kundi la East African Melody
MKURUGENZI Mipango na mtunzi mkubwa wa nyimbo za kundi kongwe la East African Melody, Shaaban Lamania , amefariki alfajiri ya kuamkia leo.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa fedha wa kundi hilo, Ashraf Mohamed, msiba uko Mbagala Kiburugwa, jijini Dar es Salaam.

Ashraf amesema mipango ya mazishi inaendelea na watatoa taarifa baadae kuhusu muda na siku ya mazishi.

Lamania ambaye amekuwa nje ya jukwaa kwa muda mrefu kutokana na ugonjwa wa kupooza, atakumbukwa kwa tungo zake nyingi ambazo hadi leo hii bado zinaendelea kulibeba kundi la Melody.

Miongoni mwa tungo zake kali ni pamoja na “Utalijua jiji” na “Mwanamke khulka”.

Mbali na utunzi, Lamania pia alikuwa mpigaji mahiri wa gitaa la solo.
‘Hakika sisi ni wa Mungu na kwake ni marejeo’.

Kwa hisani ya Saluti5...The screen masters..... 



Sunday 13 January 2013

JIANDAE KULISHWA BATA KIAINA YAKE KUTOKA KWA OFFSIDE TRICK........

Offside Trick
Nakifungua kifua nanena yalotimia ee
Kamwe sitogombania pale nilopotokea
Nakifungua kifua nanena yalotimia ee
Kamwe sitogombania pale nilopotokea

Sili kisicholika ingawa kitu jamali
Na vyema kimepikika na kurashiwa asali
Madamu ni cha shirika kula sitokubali
Kamwe sitohadaika kwa kibakuli cha wali
Kula kitu cha shirika hairidhi yangu hali

Usinipe kinyama kinukacho moshi
Mila zetu sie ni sumu ndani ya upishi ....Hheheheeee wanarejea kivyengineeeee - COMING SOON.

KHADIJA KOPA, THABIT ABDUL, HADIJA KIMOBITEL NDANI YA FITNA MPYA YA TAARAB....

NYOTA kadhaa wa miondoko ya Dansi na Taarab, wako katika mazoezi makali, kwenye ukumbi wa Equator Grill, Mtoni kwa Azizi Ally, jijini Dar es Salaam, wakiandaa albamu mpya ya taarab.

Baadhi ya nyota hao ni pamoja na Malkia wa Mipasho Khadija Kopa, Bi Mwanahawa Ally na Khadija Mnoga ‘Kimobitel’, Hassan Ali kwa upande wa waimbaji.

Katika ala, zing zong hiyo imewazoa wakali kama Thabit Abdul ‘Mkono wa Mwanaume’, Ababuu Mwana Zanzibar, Ndage Ndage, Mafloo Mzubya na Mussa Mipango.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa zing zong hiyo, Hamis Slim, mazoezi yakiwa yanaendelea vizuri, kwenye ukumbi wa Equatol Grill, huku vibao vitatu vikiwa tayari vimeshakamikamilika na kurekodiwa. 
“Vibao hivyo na waimbaji wake kwenye mabano, ni ‘Naepuka Mfarakano’ (Kimobitel), ‘Nyumba Imepata Mwenyewe’ (Mwanahawa Ally) pamoja na ‘Fahari ya Mwanamke’ (Khadija Kopa).

Kumekuwa shaka kuwa huenda mkusanyiko ni ‘fitna’ mpya itakayopelea kuzaliwa kwa bendi mpya ya taarab, kama ambayo historia inavyotukumbusha namna bendi za Zanzibar Stars, Five Stars na Mashauzi Classic zilivyoanzishwa kutokana na mikusanyiko kama hii.

Mkusanyiko huu utaunda albam yenye jumla ya sita huku jina la bendi hiyo isiyo rasmi likijulikana kama G-FiveModern Taarab.

Kwa hisani ya Saluti5.....The screen masters
 




Thursday 10 January 2013

NEW ZANZIBAR STARS INAREJEA KIVYENGINEEE......

KUNDI la miondoko ya taarab la New Zanzibar Stars limesukwa upya ili kuweza kupiga muziki wa ushindani.
 
New Zanzibar Stars ambalo katika miezi ya hivi karibuni, lilidorora na kupotea kwenye ushindani wa muziki, limeweka kambi yake Kawe jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Masae Garden View na litakuwa likitumbuiza ukumbini hapo kila Jumatano.

Mmoja wa viongozi wa kundi hilo, Rajab Kondo ambaye ni mahiri katika ucharazaji gitaa la bass, amewataka wale wote ambao walidhani New Zanzibar Stars imekufa, wafike kwa wingi Massae Garden, Jumatano hii (leo) na kila Jumatano ili wapate burudani iliyokwenda shule.

“Tumeisuka upya bendi yetu tukiwa na mseto wa wanamuziki chipukizi na wazoefu” alisema Kondo ambaye anasaidiwa na mpiga kinanda Ndagendage katika kuongoza jahazi la New Zanzibar Stars. 

Courtesy of Saluti5.....


Monday 7 January 2013

JOKHA AKIRI KUMCHAMBA LEILA RASHID........KASHESHEEEEE!!!

MWIMBAJI wa kundi la T-Moto Modern Taarab, Jokha Kassim, hatimaye amekiri kuwa anampiga vijembe mwimbaji wa Jahazi Modern Taarab, Leila Rashid.

Akiongea katika kipindi cha Hot Mix cha kituo cha televisheni cha EATV (Channel 5), Ijumaa iliyopita, Jokha alisema hata hivyo vijembe hivyo ni vya kibiashara.

Mwanzoni Jokha alikataa kabisa jambo hilo, lakini baada ya kubanwa sana na mtangazaji Mwanne Othman, hatimaye mwimbaji huyo, mke wa zamani wa Mzee Yussuf alikubali kuwa ndani ya nyimbo zake kuna vijembe vilivyolengwa kwa Leila Rashid.
 
Kwa muda mrefu sasa, Jokha ameonekana kama mtu wa kusubiria nyimbo za Leyla ambaye ni mke wa Mzee Yussuf na kisha kuzijibu.
Jokha Kassim (kushoto) akiwa na Mwanne katika studio za Channel 5
Katika wimbo Langu Rohoni wa Leila kuna mstari unasema “Si kama siwezi kusema, naweza mpaka kukesha” ambapo katika wimbo mpya wa Jokha Domo la Udaku utakutana na maneno “Kama kukesha kakesha popo, itakuwa wewe muokota makopo”.

Katika Sina Muda Huo wa Leila pale panaposema “Nina hamsini zangu zinanipeleka mbio”, Jokha anajibu tena katika Domo la udaku: “Huna hamsini wala mia”.

Kwenye wimbo mwingine wa Jokha, Unavyojidhani Hufanani, mwimbaji huyo anahoji: “Hicho cheo cha kujipachika alokupa ni nani” inaaminika ni kijiembe kwa Leila ambaye amekuwa akijulikana pia kwa jina la Malkia.

Courtesy of Saluti5....


Sunday 6 January 2013

MY CHOICE 2013..........NA MAMBO BADOOO....!!

Uzinduzi wa albamu ya 9 ya JAHAZI Modern Taarab.
Toto la Matashtiti Mwa4 wa East African Radio na Lady F wa Pwani FM ndani ya Mwananyamala Dar es Salaam Tanzania.
Lady F na Hawaa wa ITV ndani ya Travertine Hotel Magomeni Dar es salaam Tanzania.
Jahazi Modern Taarab.
Lady F na kundi zima la JAHAZI.

Lady F na Malkia Leila Rashid na kunzi zima la JAHAZI.
Mfalme Mzee Yussuf akizindua rasmi album ya Wasiwasi wako....
Mfalme Mzee Yussuf akiimba LIVE wimbo wake wa Wasiwasi Wako.....
Mzee Yussuf akirindima kwa raha zake na wana kiduku...
Malkia Leila Rashid.....
Leila Rashid akiimba LIVE wimbo wake wa Sitaki Shari.....
A closer look @ Malkia Leila Rashid.....
Chiriku Original Khadija Yussuf kuelekea stejini.....
Khadija Yussuf akirindima na wana kiduku na wimbo wake Mambo Bado....
Mama shughuli Fatma Ali....
Fatma Ali jukwaani akiimba wimbo wake Hata Bado Hujanuna....
Mtoto Pori Moh'd Ali akiimba wake LIVE kwa jina la Kazi Mnayo....
Mwamuonaje Mtoto Pori akirindima na mashabik wake jukwaani.....
Rahma Machupa...
Mcharuko wa ukwee Fatma Mahmud....
Tabasamu la kumwaga Jokha Kassim, Mkurugenzi wa T Moto Amin Salmin na Lady F....
Lady F na kundi zima la T Moto Dar es Salaam Tanzania....