MWIMBAJI mwandamizi wa kundi la Jahazi Modern Taarab, Hadija Yussuf kwa mara nyingine tena amejifungua lakini mtoto amekuwa si rizki.
Hadija Yussuf alijifungua mtoto wa kiume katika hospitali ya Muhimbili leo asubuhi lakini mtoto huyo alifariki muda mfupi baadae.
Mume wa Hadija Yussuf, Khatib ameiambia mtandao wa Saluti5 kuwa mazishi ya kichanga hicho yamefanyika mchana huu kwenye makaburi ya Tambaza jijini Dar es Salaam.
Hii inakuwa ni mara ya nne kwa Hadija Yussuf (pichani) kufiwa na mtoto wakati wa kujifungua, mara ya mwisho ilikuwa ni katikati ya mwaka jana ambapo aljifungua kwa njia ya operesheni lakini mtoto akafariki.
Awali mwimbaji huyo alishauriwa na madaktari kupumzika kubeba mimba angalau kwa miaka miwili au mitatu jambo ambalo Hadija Yussuf ameshindwa kulitekeleza.
Moja ya sababu kadhaa zinazotajwa kuwa tatizo kwa Hadija Yussuf ni unene pamoja na uzito mkubwa.
Aidha wataalam wa mambo ya uzazi wanasema lilikuwa ni jambo la hatari kwa mwimbaji huyo kubeba mimba miezi michache tu baada ya kufanyiwa operesheni.
Kwa sasa Hadija Yussuf ana mtoto mmoja tu wa kike mwenye umri wa 16 aliyezaa na Seif Magwaru, mweka hazina wa Jahazi Modern Taarab.
Kwa hisani ya Saluti5....The screen masters.