Sunday 3 March 2013

A LADY WITH CONFIDENCE - KHADIJA KOPA......

Khadija Kopa akifanya makamuzi

Bendi la Tanzania One Theatre TOT kutoka Dares salaam Tanzania lipo mazoezini kwa sasa kuandaa album zao mpya.

Katika mahojiano ya kipekee na Pwani FM, mmoja wa waimbaji katika kundi hilo, Malkia wa Mipasho Bi. Khadija Kopa amefichua kuwa moja wapo ya vibao katika album hiyo itaitwa ‘A lady With Confidence.’

“Album ndio ziko jikoni hivi sasa tunazipika na tuko katika kutizama tizama mashairi, shairi gani litamfaa mwimbaji gani ila kwa sasa tumeanza kutengeneza nyimbo kadhaa pamoja na Hemedi Omari kwahivo siwezi kusema mengi,” Akasema Khadija Kopa.

Akikichambua kibao chake kipya kilichorushwa hewani kwa mara ya kwanza jijini Mombasa Kenya kupitia Pwani FM Bi. Khadija alisema;

“Nyimbo hii inazungumzia jinsi ya kumwelekeza mwanamke ili amvutie mumewe, Hii nyimbo kama ya mafunzo upande mwingine na mwanamke anatakiwa awe na maneno mazuri kwa mumewe, Mwanamke kila wakati anatakiwa awe smart mbele ya mumewe sababu kujipodoa sio ujinga wala sio ubishoo ni fakhari ya mwanamke na tunastahili tuwasikilize waume zetu tuzungumze na wao vizuri tuwapeti peti unajua mwanamume ni kama mtoto mdogo sio anatakiwa kubembelezwa,” Alisema Commando wa uhakika Bi. Khadija Kopa.

1 comment:

  1. hii a lady with confidence ndio ''fakhari ya mwanamke'' au ni nyimbo mbili tofauti

    ReplyDelete