Sunday 10 March 2013

FUNGA KAZI/5 STARS KUIBUA ALBAM MPYA HIVI KARIBUNI.....

Funga Kazi Modern Taarab
KUNDI jipya la mipasho kutoka Dar es Salaam Tanzania, Funga Kazi Modern Taarab, linatarajiwa kuibuka na album ya pili hivi karibuni.

Baadhi ya vibao vitakavyokuwemo katika album hiyo ni kile kinachokwenda kwa jina la 'Udugu Kazi' kitakachoimbwa na Sheshi Beshi Zainab Machupa chini ya wanamuziki mahiri, Omar Kisila, Ramadhan Kisolo na Mussa Bass.

Mkurugenzi Mkuu wa Funga Kazi, Karya Temba ‘Kapteni Temba anadokeza kuwa kibao hicho ni maandalizi ya albamu yao mpya inayotarajiwa kutinga sokoni baadaye mwaka huu.

“Kibao hicho naamini kitafanikiwa vilivyo kuwashika mashabiki pamoja na wapenzi wetu wengi, kutokana na namna kilivyobeba ujumbe mzito na mpangilio mzuri wa vyombo,” anasema Temba. 

Haya yanajiri baada ya bendi hilo kukamilisha album yao ya kwanza kwa kina la 'Funga Kazi.'

5 Stars Modern Taarab
Na huku hayo yakijiri....Kundi lililosukwa upya hivi karibuni la 5 stars pia linapanga kupakua vibao vipya hivi karibuni.

Vibao vitakavyokuwa katika album hiyo mpya ni pamoja na ‘Ukurasa Mpya’ (Ally J), ‘Mwomba Mungu Hatoki Mtupu’ (Mwanahawa Ally) na ‘Jipange Upya’ (Mariam Hamdan).

Pia kundi hilo linapanga kujitambulisha rasmi mwezi ujao sambamba na kuzindua album hiyo mpya.  

Additional Information....Saluti5 (The screen masters) 


No comments:

Post a Comment