KUNDI
la Five Stars Modern Taarab lililoko Dar es Salaam Tanzania wiki jana lilitangaza rasmi kikosi chake
na kuwataka wapenzi wa muziki wa taarab wakae mkao wa kula.
Wasanii
wapya wa kundi hilo walitajwa kwenye mkutano wa waandishi wa habari
katika hotel ya Lamada ambapo Ali Jay alikuwa ni msemaji wa wasanii huku
Jumanne Ulaya “J four” anakuwa mkuu wa juwkaa.
Wasanii
wapya waliotajwa jana na bendi zao kwenye mabano ni Jumanne Ulaya
(Msanii huru), Bi Mwanahawa Ali (East African Melody), Thabit Abdul
(Mashauzi Classic / TOT Taarab) na Sabah Muchacho (Msanii huru).
Wengine
ni Hammer Q (Offside Trick), Mosi Suleiman (Msanii huru), Mariam Amdani
(East African Melody), Mariam BSS (Kings Modern Taarab), Mauwa Teggo na
Yussuf Teggo (Coast Modern Taarab).
Ali
Jay alisema kwasasa kilichobakia ni kwa wanamuziki hao wapya pamoja na
wale wa zamani kuingia kambini kwaajili ya kutengeneza nyimbo mpya
zitakazo tikisa ulimwengu wa wapenda taarab.
Naye
Sharks ambaye ndie mmliki mpya wa kundi hilo, alisema kundi lake halina
mpango wa kuanzisha malumbano na kundi lolote la taarab na litajitahidi
kukaribisha ushirikiano na vikundi shindani kadri iwezekanavyo.
Kwa hisani ya Saluti5....The Screen Masters.