Monday 25 February 2013

KHADIJA KOPA AIBUKA NA KIBAO KIPYA MWAKA WA 2013......

Malkia wa mipasho Bi. Khadija Kopa commando wa uhakika kutoka Dar es Salaam Tanzania ameibuka na kibao kipya mwaka huu kwa jina la Fakhari ya Mwanamke na tayari kimeanza kuskika kupitia vituo mbali mbali vya radio ikiwemo Pwani FM.

Ni mojawapo ya vibao vipya vinavyoundwa kwa sasa chini ya bendi lisilo rasmi la G5 lililoko Dar es Salaam Tanzania. 

G Five ambalo limeundwa na wasanii wa bendi tofauti kama vile TOT Taarab, Mashauzi Classic, Jahazi Modern Taarab, Five Stars na New Zanzibar Stars, limetengeneza jumla ya nyimbo sita.

Kumekuwa na shaka kuwa huenda mkusanyiko huo ni ‘fitna’ mpya itakayopelea kuzaliwa kwa bendi mpya ya taarab, kama ambayo historia inavyotukumbusha namna bendi za Zanzibar Stars, Five Stars na Mashauzi Classic zilivyoanzishwa kutokana na mikusanyiko kama hii.

Mkusanyiko huu utaunda albam yenye jumla ya nyimbo sita.

Huku hayo yakijiri....
 
Bendi la T Moto tayari limekamilisha album yao ya tatu na kwa sasa linamalizia malizia vibao vitakavyokuwepo ndani.

Kulingana na mkurugenzi wa kundi hilo Amin Salmin, wanapanga kuzitambulisha nyimbo hizo katika vituo vya radio mbali mbali hivi karibuni.

Hii itakuwa albamu yao ya tatu baada ya kutambulisha ‘Domo la udaku’ na ‘Aliyeniumba Hajanikosea’.

1 comment: