Sunday 24 February 2013

FIVE STARS YATANGAZA KIKOSI CHAKE KIPYA.....

KUNDI la Five Stars Modern Taarab lililoko Dar es Salaam Tanzania wiki jana lilitangaza rasmi kikosi chake na kuwataka wapenzi wa muziki wa taarab wakae mkao wa kula.

Wasanii wapya wa kundi hilo walitajwa kwenye mkutano wa waandishi wa habari katika hotel ya Lamada ambapo Ali Jay alikuwa ni msemaji wa wasanii huku Jumanne Ulaya “J four” anakuwa mkuu wa juwkaa.

Wasanii wapya waliotajwa jana na bendi zao kwenye mabano ni Jumanne Ulaya (Msanii huru), Bi Mwanahawa Ali (East African Melody), Thabit Abdul (Mashauzi Classic / TOT Taarab) na Sabah Muchacho (Msanii huru).

Wengine ni Hammer Q (Offside Trick), Mosi Suleiman (Msanii huru), Mariam Amdani (East African Melody), Mariam BSS (Kings Modern Taarab), Mauwa Teggo na Yussuf Teggo (Coast Modern Taarab).

Ali Jay alisema kwasasa kilichobakia ni kwa wanamuziki hao wapya pamoja na wale wa zamani kuingia kambini kwaajili ya kutengeneza nyimbo mpya zitakazo tikisa ulimwengu wa wapenda taarab.

Naye Sharks ambaye ndie mmliki mpya wa kundi hilo, alisema kundi lake halina mpango wa kuanzisha malumbano na kundi lolote la taarab na litajitahidi kukaribisha ushirikiano na vikundi shindani kadri iwezekanavyo.

Kwa hisani ya Saluti5....The Screen Masters.

No comments:

Post a Comment