Tuesday 9 October 2012

Bendi la Mashauzi Classic (Wakali wa kujiachia) limekamilisha album yake mpya kwa jina la 'Viwavi Jeshi.'

Album hiyo ina vibao vinne ndani ikiwemo kibao cha 'Viwavi Jeshi' kilichoimbwa na Bi. Isha Ramadhan, 'La Mungu halina mwamuzi' by Aisha Othman, 'Sitosahau yalionikuta' by Abdul Malik na 'Sijamuona kati yenu' by Rukia Juma.

Inasemekana pia kanda ya video ya album hiyo imekamilika na vibao viwili katika album hiyo (Viwavi Jeshi by Isha Ramadhan na Sijamuona kati yenu by Rukia Juma) vimejibu kibao cha 'Funga Kazi' kilichoimbwa na Madada watatu kutoka Machupas Family.

Hivi karibuni Bi. Isha Ramadhan alipinga madai hayo na kusema kuwa hajamkusudia mtu lakini kama wenyewe wanavyosema 'Si bure iko kitu.'


Huko hayo yakijiri...Mwanamuziki mahiri katika tasnia ya taarab Bi. Mariam Khamis anatarajiwa kujifungua hivi karibuni.

Muimbaji huyo anayetamba kwa kibao chake 'Fisadi mambo leo' amewahi kuimbia kundi la Five Stars, East African Melody, Zanzibar Stars na TOT.

Baadhi ya vibao alivyotamba navyo katika vikundi hivyo ni pamoja na ‘Huliwezi bifu’, ‘Raha ya mapenzi’ na ‘Ndo basi tena’.

Kutoka hapa tunamtakia kila la kheri katika maisha yake.





 

No comments:

Post a Comment