Monday 15 October 2012

DR. MALIK AFANYIWA UPASUAJI.......

Sultwan wa Mirindimo Dr. Malik anaendelea kupata afueni nyumbani kwake baada ya kufanyiwa upasuaji wa 'Haniya' katika hospitali ya Pandya wiki iliopita.

Akizungumza na Blog hii kwa njia ya simu, Dr. Malik anasema alifanyiwa upasuaji huo baada ya kukumbwa na matatizo ya kiafya.

"Nimekuwa napata maumivu sana katika sehemu ya mshipa wa mguu hivi karibuni na kutokana na maumivu hayo ndio nikaenda kufanyiwa checking katika hospitali ya pandya wiki iliopita, Baada ya kutizamwa na daktari ndio akaamua hakuna njia nyingine mpaka upasuaji na ndio hapo nikafanyiwa upasuaji wa 'haniya' na hadi kufikia sasa naendelea kusikia nafuu," Anasema Dr. Malik.

Malik ni mmoja kati wasanii wa Mombasa wanaokuwa kwa kasi sana  katika tasnia ya taarab kutokana na vibao vyake kama 'Give us Time' alichomshirikisha Malkia wa Mipasho Bi. Khadija Kopa, 'Full Confidence', 'No Network' alivyoimba mwenyewe miongoni mwa vibao vingine vya taarab.

Kutoka hapa tunamtakia afueni ya haraka....

No comments:

Post a Comment