Thursday 18 October 2012

PONGEZI KWA MR. & MRS SAIF ALI KHAN....

Ni wazi sasa kuwa wawili hawa ni MUME na MKE rasmi katika ulimwengu wa Bollywood.

Si mwengine ni actor Seif Ali Khan na mkewe actress Kareena Kapoor Khan.

Wawili hao waliamua kufunga pingu za maisha wiki hii huko nchini India baada ya kuwa katika uhusiano wa kimapenzi kwa zaidi ya miaka mitano.

Hii itakuwa mara ya pili kwa actor Seif Ali Khan kufunga ndoa baada ya kutengana na mkewe wa kwanza actress Amrita Singh.

Kutoka hapa tunawapa pongezi na kuwatakia kila la kheri katika maisha yao ya usoni.  

No comments:

Post a Comment