Tuesday 9 October 2012

T MOTO KUIBUKA NA ALBUM YA TATU - AMIN SALMIN....

Bendi linalokuja kwa kasi sana katika tasnia ya taarab la Tanzania Moto (T Moto) linajiandaa kuunda album yake ya tatu baada ya kukamilisha album yao ya pili inayojulikana kama 'Domo la Udaku.'

Kulingana na mkurugenzi wa bendi hilo Amin Salmin, miongoni mwa vibao vitakavyokuwepo katika album hiyo ni kile kitakachoimbwa na Tabasamu la kumwaga Bi. Jokha Kassim kinachoitwa 'Mungu si Miungu.'

Amin amefichua kuwa bendi hilo limerudi tena kwa upya na lipo imara sasa na zaidi kikazi baada ya kusambaratika kwa muda mrefu tangu lilipoibuka na album yao ya kwanza inayojulikana kama 'Aliyeniumba Hajanikosea.'

Pia Amin amesema kuwa bendi hilo linajipanga kwa uzinduzi rasmi wa album yao ya pili (Domo la Udaku) hapa mjini Mombasa hivi karibuni.

Album hiyo ya pili ina jumla ya vibao vitano ikiwemo 'Domo la udaku' kilichoimbwa na Jokha Kassim, 'Sio daktari wa mapenzi' by Nassor Hussein Cholo, 'Mwanamke Hashuo' by Shinuna Kassim, 'Ubaya una mwisho wake' by Aisha Masanja na 'Behind the scene' by Nyawana Fundikira.


No comments:

Post a Comment