Sunday 30 September 2012

MZEE YUSSUF NA KHADIJA KOPA KUKUTANA ANA KWA ANA USIKU WA LEO....

Macho yote usiku huu wa leo yatakuwa kwa mahasimu wawili katika tasnia ya taarab yaani Mfalme Mzee Yussuf na Malkia wa Mipasho Bi. Khadija Kopa watakapokuwa wanashiriki katika onyesho la aina yake katika ukumbi wa Travertine Hotel Magomeni huko jijini Dares Salaam Tanzania.

Onyesho hilo lililodhaminiwa na mtangazaji wa kituo cha radio Times (Tanzania) kwa jina la 'Dida' linatarajiwa kuanza saa tatu usiku wa leo mpaka cheee na litawashirikisha wasanii kibao wakali akiwemo Chidi Benz.

Haya yanajiri huku mambo yakionekana sio shwari kati ya Big Daddy A.K.A Mfalme Mzee Yussuf na Malkia wa Mipasho Bi. Khadija Kopa....

No comments:

Post a Comment