Tuesday 4 September 2012

“URAFIKI WETU NI SPESHELI” – AFICHUA DEEPIKA PADUKONE….

Actor Ranbir Kapoor & Actress Deepika Padukone.


Muigizaji mashuhuri (Actress) katika ulimwengu wa Bollywood Deepika Padukone amekanusha madai ya kuwa anapanga mikakati ya kuhuisha uhusiano wake wa kimapenzi na Actor Ranbir Kapoor.

Deepika amedokeza kuwa hayupo na nia kama hiyo kwani uhusiano uliopo kati yao ni wa kirafiki na kwa sasa anajishughulisha zaidi na kazi yake ya uigizaji.

Itakumbukwa wakati mmoja kuwa wawili hao, walikuwa wapenzi kabla ya kuvunjika kwa uhusiano wao kutokana na madai kuwa Actor Ranbir Kapoor alikuwa na mpango wa kando.

Wawili hao sasa wamepatana na wanatarajiwa kuektisha filamu mpya ya kihindi inayojulikana kama ‘Yeh Jawani Hai Deewani.’

Haya yanajiri baada ya wawili hao kuonekana pamoja katika maeneo mbali mbali nchini India.

Huku hayo yakijiri…Inasemekana kwamba uhusiano kati ya Playboy of Bollywood Actor Ranbir Kapoor na Actress Katrina Kaif umeanza kunukia tena.

Duru zinaarifu kuwa wawili hao wamekuwa wakionekana sana pamoja hivi karibuni kwaraha zao.

No comments:

Post a Comment