Friday 7 September 2012

MWA4 AJIONDOA JAHAZI.....


Mwanne Othman maarufu kama Mwa4 amejiondoa rasmi katika kundi la Jahazi Modern Taarab kuendeleza majukumu yake katika fani ya utangazaji.

Akithibitisha hayo, Mwanne amedokeza kuwa uamuzi huo umetokana na majukumu yaliomwandama katika sekta ya utangazaji ila kwa sasa ataendelea na kuimba ngoma za mduara kiasi.

Kwa sasa Mwanne Othman ni mtangazaji wa kipindi cha taarab kinachoitwa 'Tam Tam za Mwambao' katika East African Radio nchini Tanzania na pia ameibuka na ngoma mpya ya mduara akishirikiana na msanii chupukizi Meddy kinachoitwa 'Dume Mashauzi.'

No comments:

Post a Comment