Tuesday 18 September 2012

AT KUIBUKA NA VIBAO VIPYA MWEZI UJAO.....


Ali Ramadhan maarufu kama AT anatarajiwa kuibuka na vibao vipya viwili vya mduara hivi karibuni.


Akizungumza na Pwani FM, AT amesema kibao kimoja kitaitwa bahati na atamshirikisha Mfalme Mzee Yussuf na kingine chaitwa ‘Hana haya’ ambapo atamshirikisha Malkia wa mipasho Bi. Khadija Kopa.


AT amefichua kuwa vibao hivo vitakamilika mwezi ujao na utavisikia kwa mara ya kwanza hapa Pwani FM.


Wakati huo huo pia AT alizungumzia kuhusiana na bifu lake na Offside Trick, na amesema kuwa hamna bifu kati yao ila kila mmoja kaamua kufanya kazi kivyake vyake.

No comments:

Post a Comment