Tuesday 4 September 2012

BI. KIDUDE HAJAFARIKI....

Fatuma Binti Baraka A.K.A Bi. Kidude
"Kuna watu ikishafika usiku tu huwa wanawaza wakiamka asubuhi watoke na jambo gani la uzushi ili mradi tu wazushe na litaenea jambo hilo mpaka litaaminika katika jamii."

Maneno haya ni kuhusiana na hili suala la kuzushiwa kufa kwa Muimbaji nguli mwandamizi kabisa katika tasnia ya taarab. 


Binafsi nimezungumza na Mzee Yussuf ambaye ni mjukuu wa Bi Kidude, alikanusha habari hizo na kusema kuwa anaendelea kupata afueni hospitalini baada ya kulazwa kutokana na maradhi ya sukari na shinikizo la damu (Pressure), lakini habari ambazo zipo hivi sasa si za kweli bali ni uzushi mtupu.

No comments:

Post a Comment