Sunday 30 September 2012

VIDYA BALAN KUOLEWA NA SIDDHARTH ROY KAPUR MWEZI DISEMBA...


Kila mmoja katika ulimwengu wa Bollywood yuko katika pilkapilka ya kutafuta mchumba.

Baada ya Actor Saif Ali Khan na mwenzake Kareena Kapoor ambao wanaoana hivi karibuni, sasa inaonekana ni wakati wa actress Vidya Balan naye lakini na nani?

Si mwengine ila ni Siddharth Roy Kapur kama vile mnavyomuona hapo juu katika picha.

Wawili hao wamekuwa katika uhusiano wa kimapenzi kwa muda mrefu na sasa wanataka kuboresha zaidi uhusiano wao na duru zinasema kwamba huenda wakafunga ndoa mwezi Disemba mwaka huu.

Bi. Vidya Balan anasema, “I do believe in the institution of marriage. I will not ignore it for a long time. I will definitely get married.”

Japo hajazungumzia zaidi kuhusu tarehe ya harusi hiyo lakini mwezi Mei Bi. Vidya alithibitisha kuwa katika uhusiano na Siddharth.

 “I will admit that I am dating him but not beyond that,” Anasema Vidya Balan.

No comments:

Post a Comment