Thursday 20 September 2012

5 STARS YAIBUKA NA ALBUM MPYA YA 'HUNA JIPYA'...

Bendi la 5 stars limerudi kivyingine na sasa limeibuka na album mpya kwa jina la ‘Huna Jipya.’


Kulingana na mkurugenzi wa bendi Ally Juma ‘J’, albamu hiyo itakuwa na vibao vine ikiwemo jina la albamu ‘Huna jipya’  itakayoimbwa na Bi. Zena Mohammed, ‘Kusema Twasema’ by Mwamvita Shaib, ‘Kazi na dawa’ by Hammer Q miongoni mwa vibao vingine.

Tayari vibao hivyo vimeanza kuskika katika vituo mbali mbali vya radio na albamu hiyo itazinduliwa mwezi Novemba Mwaka huu.

Huku hayo yakijiri….Bendi hilo limekiri kujibu kibao cha ‘Nilijua mtasema’ by Chiriku original Bi. Khadija Yusuf kutoka Jahazi na kile kibao ‘Kusema Twasema’ by Mwamvita Shaib kutoka 5 stars.

Mkurugenzi wa bendi hilo Ally J amethibitisha hayo huku akisema kuwa hatua hiyo ilitokana na bendi hilo kujipa umaarufu zaidi na hali ya kibiashara.

‘’Ndio, tumejibu kibao cha ‘Nilijua Mtasema’ na ‘Kusema Twasema’ na sio kwa ubaya bali ni katika hali ya kibiashara na pia kujipatia umaarufu zaidi ila hatutaji jina bali tunaangalia na macho tu,”Alisema Ally J.

Hata hivyo Ally J amesema kuwa hamna bifu linaloendelea kati ya bendi la 5 Stars na Jahazi.

Huku hayo yakijiri, tayari kanda ya video ya album hiyo imekamilika...Kazi kwako sasa.

No comments:

Post a Comment