Sunday 16 September 2012

MFALME MZEE YUSSUF KUFANYA ONYESHO LA KIPEKEE NCHINI CANADA.....



Big Daddy A.K.A Mfalme Mzee Yussuf anatarajiwa kufanya onyesho la aina yake nchini Canada mwezi ujao.

Onyesho hilo la siku mbili, litafanyika kufuatia mwaliko kutoka kwa wapenzi wa kundi hilo lenye mashabiki katika kila kona ya dunia.

Haya yanajiri huku bendi la jahazi likijitayarisha kukamilisha album yao mpya kwa jina la ‘Wasiwasi wako ndio maradhi yako’ na baadhi ya nyimbo katika album hiyo ni pamoja na Nipe stara, Kazi mnayo, Hata bado hamjanuna miongoni mwa vibao vingine.

Album hiyo itazinduliwa mwishoni mwa mwaka huu.

No comments:

Post a Comment