Friday 14 September 2012

HIVI NDIVYO MAMBO YALIVYOKUWA KATIKA BIRTHDAY YA RAHMA MACHUPA HUKO TRAVERTINE HOTEL TANZANIA...

 Vinywaji vikiandaliwa.
Hapo ni Amigo, Mohamed Ali na Rahma Machupa wakianza kukata keki.
Kama kawaida wakijadiliana jambo kabla ya kukata keki.
Rahma Machupa akianza kukata keki.
Mohamed Ali akikata keki kugawa kwa mashabiki.
Keki ikiwekwa kwenye sahani.

Imependeza.
Rahma akianza kuwalisha keki mashabiki wa Jahazi.
Keki ikiendelea kukatwa.
Chukua na wewe.
Subiri tuonje na sisi kwanza.
Rahma akimlisha Mohamed Ali kipande cha keki.
 Ikiwa imehifadhiwa vizuri nadhani mumeiona ilivyotengenezwa vizuri.
Haya sasa mate yanawatoka...mumeiona?
Mtoto pori akianda maakuli.
Muimbaji anayechipukia kwa kasi katika bendi la Jahazi Mordern Taarab (Rahma Machupa) safari hii aliamua kusherehekea siku yake ya kuzaliwa hadharani katika ukumbi wa Travetine Hotel huko Tanzania.

Katika sherehe hiyo fupi, mashabiki wa Jahazi pamoja na waimbaji wa kundi hilo, walipata fursa ya kula keki na vinywaji mbalimbali vilivyoandaliwa na muimbaji huo.

Muimbaji huyo ambaye aliamua kuvaa vazi la kabila la kimasai alikuwa anatimiza miaka .... tangu kuzaliwa kwake, na pia kuwashirikisha mashabiki wake katika sherehe hiyo iliyovutia mashabiki wengi.

Kiongozi wa kundi la Jahazi 'Big daddy' Mzee Yussuf alimpongeza muimbaji huyo na kumtakia kheri na fanaka katika maisha yake.

No comments:

Post a Comment