Tuesday 4 September 2012

SHANGWE, VIFIJO NA NDEREMO ZATANDA KATIKA ULIMWENGU WA BOLLYWOOD KUFUATIA HARUSI YA KAREENA KAPOOR

Actress Karishma Kapoor

Shangwe, vifijo na nderemo zimeanza kutanda katika ulimwengu wa Bollywood kufuatia bonge la harusi inayotarajiwa kati ya Actor Saif Ali Khan na Actress Kareena Kapoor.

Mmoja kati yao ni dadake Bi. Harusi mtarajiwa, Actress Karishma Kapoor.

Alipoulizwa kuhusu tarehe rasmi ya harusi ya dadake, Karishma alidinda kutoa jibu kamili na kusema kuwa aliye na jibu kamili ni dadake Kareena Kapoor ambaye hivi karibuni atakuwa katika pilkapilka ya kuzindua filamu yake mpya inayoitwa ‘Heroine.’

Wakati huo huo Karishma amefichua kuwa kwa sasa anapumzika na huenda akajitosa katika uigizaji kwenye ulimwengu wa Bollywood mwakani.

Karishma Kapoor ni mmoja kati ya actress machachari aliye enziwa na wengi katika ulimwengu wa Bollywood kutokana na filamu zake kama ‘Coolie No.1’, ‘Dil To Pagal Hai’, ‘Hero No. 1’, miongoni mwa filamu nyingine za kihindi.

No comments:

Post a Comment