Sunday 30 September 2012

THABIT ABDUL KUFUNGA NDOA NA MWANAHAWA ALI CHIPOLOPOLO.....

Baada ya kuhusishwa kuwa na Jike la simba yaani Bi. Isha Ramadhan mara nyingi, Profesa wa Keybord Thabit Abdul Mkono wa Mwanaume Sherii nangai wa Mashauzi Classic anatarajia kumuoa muimbaji kutoka Kings Modern Taarab Mwanahawa Ally Chipolopolo A.K.A Rais wa machipukizi wa taarab Tanzania.

Akizungumza na Mwa4 kupitia kipindi cha 'Tam Tam za Mwambao', Thabit alisema tayari ameshatoa barua na sasa wapo katika maandalizi ya ndoa yao.
Pia Thabit anasema ana bonge la SURPRISE kwa kila mmoja ifikiapo mwezi Novemba mwaka huu.
Wakati huo huo wawili hao wameibuka na kibao kipya kwa jina la 'Hatuna Habari' kudhihirisha wazi wazi mapenzi yao yaani siku hizi mambo hadharani ama vipi?...Kutoka hapa tunawatakia kila la kheri katika maisha yao.
 

No comments:

Post a Comment