Monday 10 September 2012

YALIYOMO NDANI YA BENDI LA MASHAUZI CLASSIC...


Mkurugenzi wa bendi la Mashauzi Classic Bi. Isha ramadhan amepinga madai ya kujibu kibao cha ‘Funga Kazi by 3 dada wa Machupas Family.

Akizungumza kupitia kipindi kimoja cha taarab nchini' Rusha Roho' , Mashauzi amesema hajamuimba mtu, hana mda na mtu na wala hao Machupas family hawajafikia hadhi yake ya kujibizana nao.

Mashauzi pia alisema hajagombana na madada hao wala kuonana nao tangu wahame katika bendi hilo.

Alifananua kuwa madada hao walijiondoa wenyewe katika bendi hilo kutokana na kukosa kufika shughulini kwa siku kadhaa.

Kwa sasa bendi hilo linapanga kuandaa albamu yao mpya inayotarajiwa kuzinduliwa mwaka ujao.

Pia Isha alidokeza kuwa hana uhusiano wowote na mpiga kinanda Thabit Abdul ila ni wa kikazi.

No comments:

Post a Comment