Thursday 6 September 2012

GUSA GUSA MINI BAND KUTAMBULISHA ALBAMU YAO YA KWANZA MWAKANI....

Bendi la GusaGusa Mini Band linajikakamua kumaliza albamu yao ya kwanza kwa jina la ‘Unajidodo Linakuchukucha.’

Tayari bendi hilo limevitambulisha vibao viwili katika album hiyo kama ‘Unajidodo Linakuchukucha’ iliyoimbwa na B52 A.K.A Bi. Afua Suleiman na ‘Mapenzi hayana formula’ kilichoimbwa na the Beauty Queen A.K.A Bi. Swabaha Salum.

Kwa sasa bendi hilo liko katika pilka pilka ya kumaliza kibao kinachofahamika kama ‘azurure’ kitakachoimbwa na Mzee Sultan na ‘Mwanagenzi’ kitakachoimbwa na chipukizi Asya Maryam.

Bendi hilo linatarajia kuzindua albamu hiyo yao ya kwanza mwakani.

No comments:

Post a Comment