Sunday 23 September 2012

TAMASHA LA 'GIVE US TIME NYT' KUFANYIKA DISEMBA....

Lady F wa ukwee-eh na Malkia wa Mipasho Bi. Khadija Kopa.
Sultan wa Mirindimo Dr. Malik.


Tamasha babkuwa la Taarab linaloitwa ‘GIVE US TIME NIGHT’ linalotarajiwa kuleta pamoja kwa mara ya kwanza mji wa Dar-es-salaam Tanzania na Mombasa Kenya katika sanaa ya burudani huenda likafanyika mwezi wa disemba mwaka huu huko mjini Mombasa.

Lengo la tamasha hilo ni kuzindua album mpya ya ‘GIVE US TIME’ iliyowaleta pamoja msanii wa Mombasa Kenya Dr.Malik na Dar es salaam Tanzania Malkia wa Mipasho Bi. Khadija Kopa.

Kulingana na Malkia wa Mipasho Bi. Khadija Kopa, kwa sasa mipangilio ya kuandaa tamasha hilo la kipekee linaendelea kati yake na Sultan wa Mirindimo Dr. Malik na kuongezea kuwa tamasha hilo litakuwa kubwa la aina yake kwani wanapanga kushirikisha mabendi tofauti katika kanda ya afrika mashariki.

Wakati huo huo, Bi. Kopa amesema pia video ya album hiyo inaandaliwa kwa sasa na itakamilika hivi karibuni na kutambulishwa rasmi wakati wa uzinduzi huo.

Album hiyo ya ‘GIVE US TIME’ ina vibao vinne ikiwemo jina la album ‘Give us time’ iliyoimbwa na Dr. Malik akimshirikisha Khadija Kopa, ‘Full confidence’ by Dr. Malik, ‘Mjini Chuo Kikuu’ by Khadija Kopa, na ‘Simtoi’ by Khadija Kopa.

No comments:

Post a Comment