Monday 10 September 2012

T MOTO IPO IMARA - ASEMA AMIN SALMIN...

Bendi la T Moto lipo imara hata baada ya kuhama kwa baadhi ya wasanii kutoka bendi hilo hadi lingine.

Mkurugenzi wa bendi hilo Amin Salmin amethibitisha kuondoka kwa Mrisho Rajab kutoka bendi hilo hadi Kings Modern Taarab.

Amin amesema, "Ndio, Mrisho Rajab aliondoka kwa ruhusa ya bendi hadi Kings Modern Taarab kutokana na mipango yake mwenyewe ila hajaondoka kwa ubaya bali alituambia mapendekezo yake nasi tukafanya mazungumzo na bendi la Kings na sasa kweli yuko Kings."

Mrisho Rajabu ni msanii wa pili kuhama bendi hilo hadi Kings baada ya Bi. Mwanahawa Ali Chipolopolo.

Kulingana na Amin, bendi la T Moto liko katika harakati ya kutambulisha albam yake ya pili hivi karibuni na linapanga kuzindua hapa Mjini Mombasa.

Baadhi ya vibao katika albamu hiyo vimeanza kusikika kupitia vituo vya radio mbali mbali ikiwemo Domo la udaku iliyoimbwa na Jokha Kassim na Hakuna Daktari wa Mapenzi iliyotiwa sauti na Nassor Cholo.

Vibao vingine katika album hiyo ni Mwanamke Hashuo by Shunayna Kassim, Behind the scenes by Nyawana na Ubaya una mwisho by Aisha Masanja na zinatarajiwa kuanza kuskika hivi karibuni kupitia kituo cha Pwani FM.

No comments:

Post a Comment