Sunday 16 September 2012

BENDI LA TOT LIPO IMARA NA KUIBUKA NA ALBAMU MPYA HIVI KARIBUNI....

Baada ya album ya 'Full Stop', sasa bendi la Tanzania One Theatre maarufu kama TOT linajiandaa kutoa albamu yao mpya hivi karibuni.

Malkia wa mipasho bibiye Khadija Kopa amesema bado jina la albamu hiyo halijajulikana na mipangilio bado inaendelea kufanikisha albamu hiyo hivi karibuni.

Miongoni mwa vibao vitakavyokuwepo katika albamu hiyo mpya ni 'Hasada yako ndio uchawi wako itakayoimbwa na Bi. Mwasiti Suleiman miongoni mwa vibao vingine.

Pia Kopa alikanusha madai ya kuwa bendi hilo linayumbayumba na kusema lipo imara na hivi karibuni tutajua mbivu na mbichi kuhusu bendi hilo na mengi zaidi atakapowasili hapa mjini Mombasa mwezi huu wa Septemba kupitia Pwani FM.

 


No comments:

Post a Comment