Sunday 23 September 2012

KANDA YA VIDEO YA 'FULL STOP' IPO TAYARI....

Kundi la Tanzania One Theatre maarufu kama TOT limeibuka na kanda ya video ya album yao ya hivi karibuni ‘Full Stop.’

Tayari kanda ya video ya albam hiyo inapatikana madukani kwa wingi na ina vibao vinne ndani yake ikiwemo kibao cha ‘Full stop’ iliyoimbwa na Khadija Kopa, ‘Unanitafuta sana’ by Mwasiti Suleiman, ‘Rudi mpenzi’ by Ally Star na ‘Tenda wema uende zako’ by Mwanamtama Amir.

Kulingana na mmoja wa wasanii katika bendi hilo malkia wa mipasho Bi. Khadija Kopa, album hiyo imejaa mapinduzi hasa katika kibao cha ‘Full stop’ ambapo anasema alishuti video hiyo kitamaduni na katika mandhari mbali mbali nchini Tanzania.

Hivyo Malkia huyo aliwaomba wapenzi na mashabiki wa muziki huo kujipatia nakala za video hiyo katika hali ya kuinua na kukuza sanaa ya burudani.

Haya yanajiri huku bendi hilo likiwa linajiandaa kuibuka na album mpya hivi karibuni.

No comments:

Post a Comment