Thursday 6 September 2012

BIFU LIMEISHA KATI YETU NA AT - OFFSIDE TRICK

 
Wakali wa ngoma za mduara afrika mashariki maarufu kama Offside Trick wamefichua kuwa bifu kati yao na msanii AT limeisha. 

Katika ziara yao hapa mjini Mombasa hivi karibuni, Lil Ghetto ambaye ni mmoja kati ya offside Trick amedokeza kuwa walikosana na AT kibiashara wala sio katika maswala ya kibinafsi. 
  
Wakati huo huo Offside Trick watatoa ngoma mpya hivi karibuni kama Kiwembe, Chatu, Mchezo wa Mombasa inayokwenda hivi " Unavitaka vya watu vyako wavibania, Mpenda vya watu na vyake pia huliwa, Nipe nikupe ndio mchezo wa Mombasa."

Wakati huo huo Hammer Q amejiunga rasmi na kundi hilo la Offside Trick ili kuchukua nafasi ya Muda Chris  aliyeamua kupumzika kutoka mziki.

Huku hayo yakijiri... Msanii Ali Ramadhan maarufu kama AT anatarajiwa kutambulisha vibao vyake vipya viwili vya mduara hivi karibuni ambapo ameshirikiana na Malkia wa Mipasho Bi. Khadija Kopa na Big Daddy Mfalme Mzee Yussuf.

No comments:

Post a Comment