Friday 7 September 2012

BI. KIDUDE AENDELEA KUPATA AFUENI....




Hali ya msanii nguli wa muziki wa taarab Fatma Baraka maarufu kama Bi Kidude inaendelea vizuri huko alikolazwa katika hospitali ya Hindu mandali iliyopo jijini Dar  es Salaaam.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa kundi la Jahazi Mordern Taarab Mfalme Mzee Yussuf ambaye pia ni mjukuu wa Bi Kidude alisema kuwa hali yake inaendelea vizuri na jana (Alhamisi) alitoka kufanyiwa vipimo, hivyo ataendelea kuwepo hospitalini hapo hadi pale hali yake itakapoimarika.


Mfalme aliongezea kuwa hajapewa nafasi ya kuzungumzia kuhusu hali yake wakati Bi. Kidude anapoendelea kupata mapumziko zaidi.

No comments:

Post a Comment