Monday 10 September 2012

: HATMA YA FATMA MCHARUKO NI IPI KWA SASA?



Fatma Mahmoud msanii wa kundi la Jahazi,  aelezea kinachomsabishia mahudhurio yake kuwa ya nadra katika shoo za bendi yake, Miezi kadhaa iliyopita alikuwa nje ya bendi takribani Mwezi mmoja akidai kuwa alikuwa anaumwa, huku tetesi zikisema kasimamishwa kwa utovu wa nidhamu.

Leo kupitia kipindi cha taarab cha ‘Kwa raha Zangu’ hapa Mombasa, Bi. Fatma amefichua kuwa kulichomsababishia mahudhurio yake kuwa nadra katika shoo za bendi yake ni kuwa alikuwa hajiskii vizuri na kwamba alichukua muda huo kujitibu homa aliyokuwa nayo.

Fatma pia amekanusha tetesi zinazosema kuwa kasimamishwa kazi katika bendi la Jahazi kutokakana na utovu wa nidhamu na kudokeza kuwa yuko kazini kama kawaida.

Mcharuko pia alisisitiza kuwa kwa sasa bado yupo ndani ya kundi la Jahazi na hatarajii kutoa ngoma mpya kwa sasa ila anawapa nafasi wenzake chipukizi.

No comments:

Post a Comment