Thursday 6 September 2012

KINGS MODERN TAARAB YAKAMILISHA ALBAMU YAO MPYA

 
Albamu mpya inayotambulika kama 'My Heart' kutoka Kings Modern Taarab imekamilika.

Kulingana na mmoja wa wasanii katika bendi hilo Hassan Ali, Albamu hiyo ina vibao vinne ikiwemo jina la albamu 'My Heart' iliyoimbwa na yeye Hassan Ali, Dunia Duara By Mwanahawa Ali Chipolopolo, Full Style By Hanifa Maulidi & Heshima yako imeshuka by Wahida dadi.


Pia Hassan anatarajiwa kuibuka na kibao chake kipya (ZING ZONG) kinachofahamika kama 'My Choice' hivi karibuni baada ya Bahati  sio wrong number na Harusi ya mwanangu ambapo alimshirikisha Jembe gumu Bi. Mwanahawa Ali.

Pia Hassan Ali amethibitisha kurudi kwa Bi. Mwanahawa Ali Chipolopolo katika bendi la Kings kutoka bendi la T Moto na kujiunga kwa Msanii Mrisho Rajab katika bendi hilo kutoka bendi la T Moto.

Je nini haswa kinachoendelea katika bendi la T Moto?

Ili kukupatia jibu...Juhudi zetu za kumtafuta mkurugenzi wa bendi la T Moto Amin Salmin bado zinaendelea .

Haya yanajiri huku bendi la T Moto likirudi kivyingine na kuibuka na vibao vipya vitano kama Domo la udaku by Jokha Kassim, Hakuna daktari wa mapenzi by Nassor Cholo, Behind the scene by Nyawana, Mwanamke hashuo by Shununa Kassim na Ubaya hauna mwisho by Aisha Masanja na tayari  vibao viwili (Domo la udaku by Jokha Kassim na Hakuna Daktari wa mapenzi by Nassor Cholo) vimeanza kuskika kupitia vituo mbali mbali vya radio.






No comments:

Post a Comment