Sunday 30 September 2012

KUNANI KATI YA HASSAN ALI NA SAIDA MASHAUZI??

Ni jambo la kawaida kwa wasanii mbali mbali katika sanaa ya burudani kujitosa katika uhusiano wa kila aina na hasa wa kimapenzi.

Na si jambo geni kwa msanii kama huyu katika tasnia ya taarab kuwa katika uhusiano kama huo na mwenzake.

Namaanisha Young Hassan Ali na Dadake Isha Ramadhan maarufu kama Saida Mashauzi.

Hassan amethibitisha kuwa wawili hao walikuwa katika uhusiano wa kimapenzi lakini kwa sasa hamna tena kitu kati yao.

Japo aliongea kwa machungu, Hassan alidinda kusimulia chanzo cha kuvunjika kwa uhusiano wake na Saida  huku duru zikiashiria kuwa kuna mtu mwengine katika maisha ya bibi huyo.

Juhudi zetu za kumtafuta Bi. Saida Mashauzi zinaendelea.....na nitakujulisha zaidi.

No comments:

Post a Comment