Wednesday 12 September 2012

BI. MWANAHAWA KUIBUKA NA KIBAO KIPYA HIVI KARIBUNI....

Bi. Mwanahawa Ali A.K.A Jembe Gumu yuko katika pilka pilka ya kutayarisha kibao chake kipya kwa jina la 'Sijawahi kukiona kidonda cha matusi.'

Akizungumza na Blog hii, Bi. Mwanahawa amesema kwa sasa yupo mazoezini na hivi karibuni atarekodi kibao hicho katika hali ya kusaidia bendi nyingine iliopo Zanzibar.

Baadhi ya mistari katika kibao hiko ni "Sijawahi kukiona kidonda cha matusi wala sijatoka kovu miye kwa kunisaliti, nawapotezea oohh nawapotezea mimi sijali nawapotezea ohhh nawapotezea hinitii magharibi ya roho."

Bi. Mwanahawa amedokeza kuwa bado kundi la East African Melody lipo imara na lina mipango ya kuzindua albamu yao inayofahamika kama 'Rabi Nilinde.'

"Melody ilikuwa izindue albamu ya 'Rabi Nilinde' lakini kutokana na kifo cha Alawy ikabidi waahirishe uzinduzi huo lakini bado wana nia ya kuzindua hivi karibuni na lipo imara bado."

Pia bendi la Melody litajitosa katika tamasha la 'Usiku wa Flavour za Dhahabu' litakalofanyika jumapili hii huko Dar live jijini Dar es salaam Tanzania.

Haya yanajiri huku Bi. Mwanahawa akimpoteza mamake mzazi mwezi uliopita...Mola ailaze roho yake mahali pema peponi na tunamtakia kila la kheri katika maisha yake.

No comments:

Post a Comment