Monday 3 September 2012

BROTHER P AIBUKA NA KIBAO KIPYA CHA MDUARA

Ali Munir Macca A.K.A Brother P
: Msanii chupukizi maarufu kama Brother P A.K.A Mfalme wa Miduara aibuka na kibao kipya cha mduara kinachofahamika kama 'Mgomba.' 

Ni mmoja kati ya wasanii wa hapa Mombasa wanaoinuka kwa kasi sana katika tasnia ya mduara na ngoma zake kama 'Sure' na 'Harusi.' 


Brother P ambaye jina lake kamili ni Ali Munir Macca amerithi kipaji cha usanii kutoka kwa babake Munir na pia amewahi kupata mafunzo kuhusu sanaa hii katika bendi la Johari Orchestra. 


Brother P ana azma ya kunogesha ngoma za mduara hapa mjini Mombasa katika siku zijazo kwa kufanya collabo na wasanii mbali mbali wa miduara kama vile Offside Trick, AT na wengineo.

1 comment:

  1. maji hufata mkondo...alianza baba ,akaja kaka mkubwa sasa nae pia kajitosa kwenye tasnia ya uimbaji..

    ReplyDelete