Monday 10 September 2012

PRINCE AMIGO KUJITOSA KATIKA MDUARA NA BONGO FLAVOUR....

Abubakar Soud maarufu kama Prince Amigo amekanusha tetesi za kulihama kundi la Jahazi Modern Taarab.

Msanii huyo kutoka bendi la Jahazi amesema hana mpango kama huo na wala hajafikiria kulihama bendi hilo linaloongozwa na Mfalme Mzee Yussuf.

Kwa sasa hajajua iwapo atashiriki katika album mpya ya Jahazi inayofahamika kama 'Wasiwasi wako ndio maradhi yako.'

Pia Amigo amefichua azma yake ya kujitosa katika Mduara na Bongo Flavour katika siku zijazo.

"Nipo katika mipangilio ya kutoa album yangu mwenyewe  hivi karibuni ila sio taarab bali nyimbo zitakuwa style ya Mduara na Bongo Flavour kwahivo waambie wakae mkao wa kula."

Msanii huyu anaendelea kuvuma katika tasnia ya taarab kutokana na vibao vyake vya taarab kama Domo Kaya, 100% na Full Shangwe.

Hivi karibuni alifunga ndoa na mpenzi wake Bi. Lisser Rahmani na tunawatakia kila la kheri katika maisha yao.

No comments:

Post a Comment