Tuesday 4 September 2012

"JAHAZI LIPO IMARA DAIMA NA LITADUMU DAIMA" - MZEE YUSUF

Big Daddy A.K.A Mfalme Mzee Yussuf

Mkurugenzi wa Jahazi Modern Taarab Mfalme Mzee Yussuf amefichua kuwa bendi la jahazi lipo imara na wala halijasambaratika kama inavyodaiwa.
Mzee Yussuf amedokeza kuwa kwa sasa mabadiliko makubwa yanafanywa katika bendi hilo na kuna baadhi ya wasanii watakaokula kalamu huku wengine wakijipatia nafasi mpya ndani ya bendi hilo japo hakutaka kuzungumzia swala hili kwa kina zaidi.

Pia Mfalme hakusita kutoa hisia zake kuhusiana na vibao kutoka bendi la T moto kama Domo la Udaku na Sio Dokta wa mapenzi vinavyodaiwa kujibu vibao kadhaa kutoka bendi la jahazi, nikimnukuu alisema "Ni masikitiko makubwa kwa hao kujibu vibao hivyo kutoka bendi la jahazi ambapo vingine vimepitwa na wakati kama kile kibao cha daktari wa mapenzi, waendelee tu ila bendi la jahazi halina mda na mtu."

Wakati huo huo Mfalme amedokeza kuwa kwa sasa bendi la Jahazi lipo katika pilkapilka za kutayarisha album yao mpya inayofahamika kama "Wasiwasi wako ndio maradhi yako" ambapo jina la albamu litatambulishwa na ye mfalme Mzee Yussuf.

Albamu hiyo itakuwa na vibao sita ikiwemo kibao kinachofahamika kama 'Sitaki Shari', 'Kazi nnayo', 'Hata bado hujanuna' miongoni mwa vibao vingine....KAA MKAO WA KULA.

No comments:

Post a Comment