Thursday 18 October 2012

OFFSIDE TRICK VS AT = COMPEEE ROHO SAFIIIII.....

Wakali wa ngoma za mduara maarufu kama 'Offside Trick' wanatarajia kuachia vibao vipya kadhaa hivi karibuni.

Baadhi ya ngoma hizo ni 'Chatu,' 'Nipe Nikupe,' 'Kiwembe' miongoni mwa vibao vingine.

Pata kusikia uhondo wa baadhi ya vibao hivi hapo chini katika blog hii....


Huku hayo yakijiri Ali Ramadhan maarufu kama AT naye anatarajiwa kuibuka na vibao vipya viwili vya mduara hivi karibuni.

Akizungumza na Pwani FM, AT amesema kibao kimoja kitaitwa 'Bahati' ambacho atamshirikisha Mfalme Mzee Yussuf na kingine kitaitwa ‘Hana haya’ atakacho mshirikisha Malkia wa mipasho Bi. Khadija Kopa.

AT amefichua kuwa vibao hivo vitakamilika mwezi huu na utavisikia kwa mara ya kwanza hapa Pwani FM.

Kando na hayo Msanii wa Mombasani wa kizazi kipya maarufu kama 'LAI' naye kajitosa katika ulimwengu wa mduara.

Ameibuka na kibao chake cha kwanza aina ya mduara kinachoitwa 'Safari' ambacho kimeanza kuskika katika vituo mbali mbali vya radio hapa mjini.

Akizungumza na Blog hii, msanii huyo amesema ameamua kufanya mabadiliko kiasi katika safu ya burudani ili kuleta raha zaidi kwa mashabik.

Haya ndio baadhi ya mistari yalioko kwenye kibao hicho..."Kama ni gari iende, kama ni ndege ipae, kama ni meli ielee ikate maji…Leo moyo wanigonga kwa wingi wangu mori nimengoja siku nyingi kuienda hii safari…Ninavyojua safari huandamwa na hatari nimebeba zana nyingi kwa lolote litonikabili…Nimeyabeba maji endapo niyahitaji jangwani, nikabeba na mwavuli mvua inyeshapo jangwani, ....Naianza kwa mguu mbele ntapata gari ndani ya maji kwa meli kwa ndege kisha nijipate hewani…"

No comments:

Post a Comment