Thursday 18 October 2012

SALMAN KHAN AKO JUU KATIKA ULIMWENGU WA BOLLYWOOD…


Una habari kuwa actor huyu yuko juu kwa sasa katika ulimwengu wa Bollywood?

Si mwengine ila ni actor Salman Khan.

Inasemekana kuwa siku hizi actor huyu anafurahia maisha baada ya kuibuka kuwa miongoni mwa waigizaji wanaopata malipo ya hali ya juu katika ulimwengu wa bollywood.

Haya yanadhihirika baada ya filamu alizoshiriki hivi karibuni kama ‘Dabangg,’ ‘Ready,’ ‘Bodyguard,’ ‘Ek Tha Tiger,’ kufanya vyema katika charti ya filamu bora.
Huku hayo yakijiri, Pia Salman Khan ameonekana sana kukerwa na uhusiano wa karibu kati ya actor Shahrukh Khan na actress Katrina Kaif.

Uhusiano kati ya wawili hao (Shahrukh Khan & Katrina Kaif) unatokana na ujio wa filamu yao mpya "Jab Tak Hain Jaan' inayotarajiwa kutoka hivi karibuni.

Duru zinasema kuwa bado Salman Khan anamuenzi Bi. Katrina Kaif zaidi ya rafiki.

Haya yanajiri huku uhusiano kati ya wawili hao (Salman Khan & Shahrukh Khan) ukiendelea kufifia....Na habari ndio hiyoooo.

No comments:

Post a Comment