“Habari ndio hiyo mwanamke mazingira mambo mengine sio
mwanamke kujipura…Hata asiwe na wowowo uzuri wa mwanamke stara....”Unamtambua bibi huyu mwenye sauti ya ningaa mashallah
ya kumtoa nyoka pangoni?
Ni mtoto wa tisa kati ya ndugu zake 13 katika familia
yake.
Amewahi kurithi kipaji cha uimbaji kutoka kwa babake
mzazi, na dadake zake ambao ni wasanii katika tasnia ya taarab kwa majina ya
Jokha Kassim kutoka bendi la T Moto na Fatma Kassim kutoka bendi la Jahazi.
Si mwengine ila ni Bi. Shinuna Kassim kutoka bendi la T
moto.
Safari ya bibi huyu ilianza mwaka wa 2011 katika kundi
la Zanzibar Njema kinachomilikiwa na Ahmed Mgeni.
Amewahi kurekodi kibao kinachoitwa ‘Sinyanyui mdomo
wangu’ na bendi hilo na tayari kimeanza kuskika katika vituo mbali mbali vya
radio.
Akizungumza na Pwani FM katika kipindi cha KWARAHA
ZANGU hii leo, Bi. Shinuna alielezea bayana kilichompeleka hadi bendi la T Moto
kwa sasa….
“Yaani sio kama labda nimeamua kuhama Zanzibar Njema
ila hilo ni bendi ambalo nimejifundishia, na ilipoanzishwa bendi la T Moto dadangu
Jokha akanipigia simu akanambia kuna bendi mdogo wangu unaonaje ukaja? Nikwambia
sawa mimi nakuskiliza wewe dadangu kwahivo mimi ndio nikajiunga na T Moto kwa
sabab ya maslahi na pia nimetokea kuipenda na wenyewe ni wastaarabu,
tunapendana wasanii wote kwahiyo mwenyewe nikaona bora tu nikae katika bendi
hili,” anasema Bi. Shunaina.
Kilichompelekea yeye hadi kujitosa katika tasnia ya taarab ni mapenzi yake mwenyewe.
“Yaani napenda sana taarab na isitoshe alianza babangu kuimba na baadaye wakaja dada zangu, nami nikaona hiki kitu kipo katika damu si unajua kitu ambacho kimetoka katika damu,” Anasema Bi. Shinuna.
Baada ya kujiunga na bendi la T Moto, Bi. Shinuna
karudi tena kivyengine na kibao chake cha pili kinachoitwa ‘Mwanamke Hashuo’
katika album ya ‘Domo la Udaku.’
“Mwanamke MASHAUZI anatakiwa mwanamke awe na hashuo,
mwanamke ukiwa una hashuo utajulikana na nani? Lakini ukiwa na hashuo kila
wakati mtu anakutaja mdomoni kila mtu itatokezea akujue, na hiyo nyimbo nimekabidhiwa
na mkurugenzi wangu akanambia umeipenda? Nikamwambia nimeipenda, Kwahiyo
nikaimba na yoyote atakayejiskia imemgusa ndio ya kwake,” Anasema Bi. Shunaina
wakati anachambua kibao chake kipya cha ‘Mwanamke Hashuo.’
Kwa sasa Bi. Shunaina hajaolewa ila kadokeza kuwa ana
mchumba na wanatarajia kufungwa pingu za maisha hivi karibuni.
No comments:
Post a Comment