Tuesday 18 December 2012

ALBUM YA 'GIVE US TIME' KUZINDULIWA RASMI HUKO CLUB TROPICANA..........

Lisemwalo lipo na kama halipo lipo njiani laja na sasa ni RASMI kwamba macho yoteee mwaka huu yatashuhudia uzinduzi wa album ya kwanza ya taarab itakayounganisha mji wa Mombasa Kenya na Dar es salaam tanzania kwa mara ya kwanza katika tasnia ya taarab.

Katika mahojiano ya kipekee na blog hii/kipindi cha taarab cha 'Kwa Raha Zangu' kupitia Pwani FM, Sultwan wa Mirindimo Dr. Malik na Malkia wa Mipasho Bi. Khadija Kopa wamefichua kuwa album hiyo kwa jina la ‘Give us Time’ itatambulishwa rasmi tarehe 31 mwezi wa disemba mwaka huu wa 2012 katika ukumbi wa Club Tropicana.

“ Ni kweli tutazindua album hiyo usiku wa tarehe 31 mwezi disemba mwaka huu katika tamasha la kufunga mwaka katika ukumbi wa Club Tropicana hapa mjini Mombasa, kwa ushirikiano na bendi la TOT (Tanzania One Theatre) kutoka Tanzania, Mombasa Stars Modern Taarab na mabendi tofauti kutoka Kenya,” Akasema Bi. Khadija Kopa.

"Kwa sasa mipangilio ya kuandaa tamasha hilo linaloanza kuanzia saa tatu usiku hadi chee la ‘Pwani/Give us time Nyt’ yamekamilika na pia tutakuwa na surprise kadha wa kadha plus kiingilio ni shillingi 300/- tu kwahivo wajitahidi wapenzi wetu waje wajionee wenyewe, " Akasema Dr. Malik.

Wameahidi kuwapa wapenzi wao burudani la ‘high class’ likalalowapa raha mpaka barabarani.

“Yaani ni wakae mkao wa kula maana safari hii tutawaacha hoi kwa kuwapa burudani spesheli 
watakalolikumbuka daima na pia nakala za cd ya album hiyo zitapatikana kwa wingi siku hiyo kwahivo wajiandae kula raha,” Akasema Khadija Kopa. 

Album hiyo ya ‘Give us Time’ ina vibao vinne ikiwemo kibao kilichobeba album cha ‘Give us time’ kilichoimbwa na Dr. Malik akimshirikisha Khadija Kopa, Full Confidence by Dr. Malik, ‘Mjini Chuo Kikuu’ by Khadija Kopa na ‘Simtoi’ by Khadija Kopa.

Itakumbukwa kwamba fikra za kuunda album hii ya ‘Give us Time’ ilitoka baada ya wawili hao (Dr. Malik & Khadija Kopa) kuhojiwa kuhusiana na swala zima la kukuza sanaa ya burudani la taarab kanda ya afrika mashariki kupitia Pwani FM katika kipindi cha taarab kinachotikisa mkoa wote wa pwani cha ‘Kwa raha zangu.’

No comments:

Post a Comment