Sunday 23 December 2012

MZEE YUSSUF AMTOLEA MBAVUNI AMIN SALMIN...

MKURUGENZI wa Jahazi Modern Taarab, Mzee Yussuf amesema wataikaribisha bendi yoyote kwenye uzinduzi wa albam yao lakini kamwe si T-Moto Modern Taarab ya Amin Salmin.

Mzee Yussuf ameimabia Saluti5 kuwa kamwe hatapiga jukwaa moja na bendi hiyo kwa vile amegundua kuwa bendi hiyo imejaa ushindani wa chuki badala ya ushindani wa maendeleo.

Jahazi wanatarajiwa kuzindua albam yao mpya “Wasi wasi wako” Jumapili ya tarehe 30 mwezi huu katika ukumbi wa Travertine Hotel, Magomeni jijini Dar es Salaam.

Kwa muda mrefu Mzee Yussuf na Amin Salmin wameripotiwa kuwa na bifu zito na hata bendi zao zilipokutana kwenye tamasha la Mitikisiko ya pwani mwezi uliopita kwenye ukumbi wa Dar Live, hali ya hewa ilichafuka na wawili hao walikaribia kutupiana makonde.

“Siwezi kupanda jukwaa moja na T-Moto, ni bendi changa inayotaka kupanda juu kwa kutumia mgongo wetu, watafute njia nyingine” alisema Mzee Yussuf na kuongeza kuwa bendi nyingine yoyote ya taarab itakayojiskia kupanda jukwaa la Jahazi siku ya uzinduzi wao, inakaribishwa sana."

Huku hayo yakijiri....Wakaazi wa mji wa Morogoro wanausubiri ujio wa kundi la Jahazi Modern Taarab kwa hamu kubwa ambapo tayari onyesho la bendi hiyo limekuwa gumzo la kila kona ya mji huo.

Jahazi Modern Taarab wanatarajiwa kufanya onyesho kubwa ndani ya ukumbi wa Savoy Hotel siku ya mkesha wa X-Mas Jumatatu 25/12/2012.

Onyesho hilo ni maalum kwa ajili ya utambulisho wa nyimbo mpya kabisa zinazounda albam mpya ya “Wasi wasi wako” yenye jumla ya nyimbo sita.

Courtesy of Salut5 


No comments:

Post a Comment