Friday 14 December 2012

KWATOKOTA KATI YA THABIT ABDUL NA MWANAHAWA ALI CHIPOLOPOLO


Baada ya tashtit zote za mjini walizokuwa wakizionyesha kudhihirisha uhusiano kati ya yao, sasa imeibuka kuwa huenda Profesa wa Keybord Thabit Abdul Mkono wa Mwanaume Sherii nangai wa Mashauzi Classic na Rais wa machipukizi wa taarab nchini Tanzania Bi. Mwanahawa Chipolopolo walitumia njia hiyo kujipatia umaarufu tu. 

Baadhi ya wadau wa taarab nchini Tanzania akiwemo Malkia wa mipasho Bi. Khadija Kopa wamestukia ishu hiyo kwa kudokeza kuwa yawezekana wawili hao walipanga mpango huo madhubuti kwa ajili ya kujifanyia promo kutokana na albamu yao ya taarab. 

Kwa sasa yasemekana kuwa Bi. Mwanahawa Chipolopolo ni mja mzito huku Thabit akiiikana mimba hiyo na kusema hajawahi kukutana naye.

Katika mahojiano katika kipindi cha ‘Hot Mix kinachorushwa na kituo cha televisheni cha EATV miezi kadhaa iliopita , Thabit aliahidi kumtolea barua ya uchumba binti huyo kwa lengo la kutaka kumuoa, na kutangaza kuwa angefanya maajabu makubwa sana kwa mpenzi wake huyo ifikiapo mwezi jana (Novemba) lakini baadaye ilikuja kufahamika kuwa angemvisha pete ya uchumba kitu ambacho hakikuwa mpaka sasa.

Juhudi zetu za kuwatafuta wawili hao zinaendelea.

Haya yanajiri huku wawili hao wakiibuka na kibao cha taarab kwa jina la 'Hatuna Habari' kudhihirisha wazi wazi mapenzi yao yaani siku hizi mambo hadharani ama vipi?...Lakini nini mbaya tena?

Additional information by Mwa4 Toto la Matashtiti.

1 comment: