Tuesday 18 December 2012

THABIT AIBUKA NA KIBAO KIPYA TEINAAAAAAAAAA.......

Hayawi hayawi mwishowe huwa, baada ya kuibuka na kibao kipya kwa jina la 'Hatuna Habari' ambapo alimshirikisha Mwanahawa Chipolopolo hivi karibuni sasa Mfalme wa kinanda Thabit Abdul ameibuka na kibao kingine kinachoitwa 'Habibi.'

Kupitia kibao hicho, Thabiti amewashikirikisha baadhi ya wasanii wa kundi la Mashauzi Classic kuleta fleva mpya katika tasnia ya taarab.


Mpiga kinanda huyo amekiimba kibao hicho kwa umahiri mkubwa, akimlalamikia kimwana, ambaye amekuwa akimtesa kimapenzi.


Juhudi za kumtafuta Thabit Abdul zinaendelea kwani amekuwa mteja hapatikani hivi karibuni na tutakapompata tutakupasha zaidi.

Wakati huo huo pia mwimbaji mkongwe wa fani hiyo, Ally Hemed Star vilevile naye hataki kushindwa na kuibuka na kibao kipya kinachokwenda kwa jina la 'Ni wewe.'

Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa Ally Star kuibuka na kibao cha taarab baada ya kuwa kimya kwa takriban miaka miwili

Kama ilivyo ada na desturi, utapata kuviskia vibao hivi kwa mara ya kwanza hivi karibuni kupitia Pwani FM...Tafrija Kipwani.

Additional Information Rusha Roho Blog...

No comments:

Post a Comment