MWIMBAJI
wa taarab na muziki wa dansi, Abdul Misambano “Super Rocks” amempongeza
mkurugenzi wa Jahazi Modern Taarab, Mzee Yussuf kwa kuthubutu na
hatimaye kufanikiwa kuunda kundi la Jahazi.
Misambano
anayelitumikia kundi la TOT, aliyasema hayo alipokuwa anahojiwa na Hawa
Hassan katika kipindi cha Sham Sham za Pwani cha ITV, Jumatatu usiku.
Alisema anampongeza kwa vile wako waimbaji wengi waliopata nafasi kama ya Mzee Yussuf lakini walishindwa kuzitimia.
Mwimbaji
huyo aliyepata kutamba na wimbo wa “Asu” aliouimba akiwa na Babloom
Modern Taarab, anamtaja Ali Hemed “Star” kama moja ya mifano yake.
“Enzi
za Ali Star, nilishuhudia mwimbaji huyo akituzwa kapu la pesa,
alikubalika sana na angeweza kabisa kuanzisha kundi lake na akafanikiwa
lakini kwa bahati mbaya hakuthubutu.
“Mzee
Yussuf alithubutu na akafanikiwa na pia ameweza kuzalisha wasanii nyota
kama Isha Mashauzi na wengine wengi, kwahiyo nampongeza sana” alisema
Misambano.
Misambano
pia alishutumu tabia ya waimbaji wa sasa wa kiume kwa kuigana sana
sauti kiasi cha kufikia hatua ya kushindwa kuwatofautisha.
“Zamani
akiimba Misambano, Hussein Kibao, Ali Star, Mohamed Mrisho au Ali
Taajiruna hutapata shida, kila mtu na sauti yake na staili yake.
Kizazi
cha mwisho kukiona kikifanya kivyo ni Mzee Yussuf na marehemu Omar
Kopa, walikuwa hawafanani, lakini baada ya hapo imekuwa taabu,
ukimsikiliza Omar Teggo na Mzee Yussuf ni mle mle hakuna tofauti.
Huyu
mtoto mpya wa Jahazi (Mohamed Ali) akiimba ni kule kule kwa Mzee, Amigo
anajaribu kubadilika lakini bado kuna sehemu anapita pale pale kwa Mzee
Yussuf, watu wanaigana sana” alisema Misambano.
|
Kundi la East African Melody |
MKURUGENZI
Mipango na mtunzi mkubwa wa nyimbo za kundi kongwe la East African
Melody, Shaaban Lamania , amefariki alfajiri ya kuamkia leo.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa fedha wa kundi hilo, Ashraf Mohamed, msiba uko Mbagala Kiburugwa, jijini Dar es Salaam.
Ashraf amesema mipango ya mazishi inaendelea na watatoa taarifa baadae kuhusu muda na siku ya mazishi.
Lamania
ambaye amekuwa nje ya jukwaa kwa muda mrefu kutokana na ugonjwa wa
kupooza, atakumbukwa kwa tungo zake nyingi ambazo hadi leo hii bado
zinaendelea kulibeba kundi la Melody.
Miongoni mwa tungo zake kali ni pamoja na “Utalijua jiji” na “Mwanamke khulka”.
Mbali na utunzi, Lamania pia alikuwa mpigaji mahiri wa gitaa la solo.
‘Hakika sisi ni wa Mungu na kwake ni marejeo’.
Kwa hisani ya Saluti5...The screen masters.....