Sunday 13 January 2013

KHADIJA KOPA, THABIT ABDUL, HADIJA KIMOBITEL NDANI YA FITNA MPYA YA TAARAB....

NYOTA kadhaa wa miondoko ya Dansi na Taarab, wako katika mazoezi makali, kwenye ukumbi wa Equator Grill, Mtoni kwa Azizi Ally, jijini Dar es Salaam, wakiandaa albamu mpya ya taarab.

Baadhi ya nyota hao ni pamoja na Malkia wa Mipasho Khadija Kopa, Bi Mwanahawa Ally na Khadija Mnoga ‘Kimobitel’, Hassan Ali kwa upande wa waimbaji.

Katika ala, zing zong hiyo imewazoa wakali kama Thabit Abdul ‘Mkono wa Mwanaume’, Ababuu Mwana Zanzibar, Ndage Ndage, Mafloo Mzubya na Mussa Mipango.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa zing zong hiyo, Hamis Slim, mazoezi yakiwa yanaendelea vizuri, kwenye ukumbi wa Equatol Grill, huku vibao vitatu vikiwa tayari vimeshakamikamilika na kurekodiwa. 
“Vibao hivyo na waimbaji wake kwenye mabano, ni ‘Naepuka Mfarakano’ (Kimobitel), ‘Nyumba Imepata Mwenyewe’ (Mwanahawa Ally) pamoja na ‘Fahari ya Mwanamke’ (Khadija Kopa).

Kumekuwa shaka kuwa huenda mkusanyiko ni ‘fitna’ mpya itakayopelea kuzaliwa kwa bendi mpya ya taarab, kama ambayo historia inavyotukumbusha namna bendi za Zanzibar Stars, Five Stars na Mashauzi Classic zilivyoanzishwa kutokana na mikusanyiko kama hii.

Mkusanyiko huu utaunda albam yenye jumla ya sita huku jina la bendi hiyo isiyo rasmi likijulikana kama G-FiveModern Taarab.

Kwa hisani ya Saluti5.....The screen masters
 




No comments:

Post a Comment